Waziri wa
maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa Iran ina
jukumu la kutekeleza katika juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji wa
Islamic State nchini Iraq na Syria.
Bwana Kerry ameliambia baraza
la usalama la umoja wa mataifa kwamba muungano wa kuliangamiza kundi
hilo una majukumu mengine mbali na hatua za kijeshi na kwamba huenda
Iran ikashirikishwa.Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imebaini kwamba wawakilishi wa Iran na wale wa Marekani wamejadiliana kuhusu tishio linalosababishwa na wapiganaji hao kandokando ya vikao vya mkutano kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.
No comments:
Post a Comment