Hayo ameyasema leo katika wilayani Bagamoyo katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo amesema bandari na viwanda hivyo vitasaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana.
"Tutafanya ujenzi wa viwanda vya kisasa katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano na tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi yote," amesema Dk. Magufuli
Aidha John Pombe Magufuli aliwanadi wagombea ubunge wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa na jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni huo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment