Pages

Wednesday, 7 October 2015

Siku Mbili za Kubadilisha Maisha ya Kijana

Kanisa la Dar Calvary Temple / T.A.G Tabata shule limeanda semina kubwa ya siku mbili kwa vijana wote wa Dar es salaam kujifunza jinsi ya kujikwamua katika uchumi na jinsi ya kuimalisha mahusiano yanayopelekea ndoa ili imsaidie kijana kujipatia maendeleo ya kimwili na kiroho.

Semina hiyo inayoanza leo na kesho imeandaliwa na Idara ya vijana(Ca's) wa kanisa la DCT chini Ron Swai ambaye ni mchungaji Kiongozi a kanisa hilo pia ni Katibu mkuu wa makanisa ya T.A.G.

Aidha katika Semina hiyo litafundishwa somo la MAHUSIANO ikiwa ni katika vipengele vifuatavyo:
~MAHUSIANO YENYE FAIDA
~KUJENGA MAHUSIANO YATAKAYOKUFANYA KUMPATA MWEZA WA KUFANANA NA WEWE YAANI MUME AU MKE MWEMA.
~MAHUSIANO YAKO NA MUNGU.
~MAHUSIANO YENYE KUKUJENGA KIROHO NA KUKUZA VIPAWA VILIVYO NDANI YAKO VIKAFANYA KAZI.
~MAHUSIANO YENYE BUBUJIKO LA ROHO MTAKATIFU NA KARAMA ZIKATENDA KAZI NDANI YAKO.
~KUFURAHIA UJANA WAKO WAKO.
~JINSI YA KUONDOA MAJERAHA,MAUMIVU,UCHUNGU ULIOTOKANA NA MAHUSIANO "UCHUMBA" KUVUNJIKA NA UKAANZA UPYA HADI KUFIKIA LENGO.
~NAMNA YA KUANZA MSHUSIANO NA MTU SAHIHI NA KUTAMBUA HUYU KWELI NI KUTOKA KWA BWANA....UPATE KUJUA,KUONA NA KUELEWA.JE HUYU NDIYE?

Upande wa pili masomo mengine itakuwa kujifunza jinsi ya "kuongezeka" katika "KUMILIKI UCHUMI"

Wakati wa ujana ndio muda muafaka wa kuanza kuishi NDOTO,MAONO,MALENGO NA MIPANGO yako.
njoo "UONGEZEKE"

~MBINU ZA KUMILIKI NA KUTAWALA UCHUMI
~NAMNA YA KUANZA BIASHARA NA KUIKUZA
~JINSI YA KUTUMIA WAZO LAKO NA KUWA UTAJIRI
~KUONGEZEKA KIMALENGO NA UBUNIFU
~KUVITUMIA VIPAWA KUWA MAFANIKIO YAKO
~KUFUFUA MAONO YAKO YALIYOKUFA KWA KUKATISHWA TAMAA,KUKWAMA SEHEMU,KUKOSA MTAJI AU BAADA YA KUSHINDWA KUENDELEA NA MASOMO.

Baada ya masomo yote vijana watapata mda wa kuuliza maswali yao yanayowatatiza na kujibiwa vizuri na walimu mahili watakaokuwepo wakifundisha katka semina.

Kila kijana atakayefika hakika atapata vitu hadimu sana na itakuwa ni mda muafaka kwa vijana kukutana na kufamiana sambamba na kujifunza mengi yahusuyo ujana katika semina hiyo itakayoanza mda wa saa 9:00 alasili na kumalizika saa 12:00 jion kwa maelezo zaidi unaweza kufungua katika mtandao na kulike page ya face book hii: dar calvary temple youth ministry.

No comments:

Post a Comment