Pages

Friday, 9 October 2015

WATUHUMIWA WA MAKOSA YA MTANDAO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao Benedic Angelo Ngonya(24)(wa kwanza kulia) anayetuhumiwa kusambaza katika mitandao  taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka. 


Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini(wa Pili kulia), Huang Kun Bing (26)Raia wa China (wa Tatu Kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza Kushoto) Hefeez Irfan (32)(wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig(41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka ya Uwizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network). 


 Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23, watuhumiwa  wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.
Source:Michuziblog.

No comments:

Post a Comment