Akizungumza na washiriki jana katika mkutano huo Rais Jakaya Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa sekta binafsi pamoja na taasisi mbalimbali zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kusaidia katika kuliletea maendeleo taifa husika.
Katika mkutano huo ambao ulikuwa na washiriki wengi kutoka mataifa mbalimbali umelenga kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusiana na kuwa wazi katika utoaji wa taarifa barani Afrika.
Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mh. Mathias Chikawe kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kwenye mkutano huo Chikawe alisema mfumo wa utoaji taarifa kwa uwazi ni mhimu kwa sababu husaidia uwazi pamoja na uwajibikaji katika nchi.
Mkutano huo mkubwa wa takwimu ulisheheni washiriki toka nchi 23 za Afrika ukiwa na malengo ya kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika.
No comments:
Post a Comment