Mbasha ambaye pia ni mume wa msanii wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, alipiga magoti na kuangua kilio nje ya mahakama baada ya kusomwa hukumu hiyo iliyomwachia huru dhidi ya tuhuma za ubakaji.
Hukumu hiyo ilisomwa jana saa 4:45 hadi saa 5:15 asubuhi na Hakimu Mkazi Flora Mgaya wa mahakama hiyo.
Hakimu alisema baada ya ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa Jamhuri na ushahidi wa mshtakiwa, mahakama imeona bila kuacha shaka hautoshelezi kumtia hatiani.
Alisema mahakama yake inamwachia huru mshtakiwa Mbasha. Mbasha alitoka kasi kwenye chumba cha mahakama na kupiga magoti huku akili kwa sauti na kusema 'Mungu amenitetea katika maisha yangu… Mungu amenilinda, ameniepusha na kwenda kuozea jela … namshukuru sana sina cha kumlipa' alisisitiza wakati akilia mahakamani hapo.
"Mniache sina kitu cha kuongea Mungu wangu yu hai amenitetea na kuniepusha na kuozea jela mimi…" alisema Mbasha huku akilia na kuzungukwa na watu pamoja na wanahabari.
Katika kesi ya msingi, ilidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment