WATU wasiojulikana wamechoma moto makanisa mtatu mjini Bukoba . Makanisa yaliyochomwa moto ni Pentecostal Assemblies of God (PAG) eneo la Buyekera, Living Water International na Evangelical Assemblies of God (EAGT) kata ya Kibeta yote ya mjini Bukoba.
Wachungaji na viongozi wa kiroho wa makanisa hayo wametoa wito kwa vyombo vya dola kuwabaini wahusika wa tukio hilo linaloashiria uvunjifu wa amani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augstine Oromi, amethbitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atatoa tamko rasmi baadaye.
Matukio ya makanisa kuchomwa yameshamiri katika Manispaa ya Bukoba, ambapo hili ni tukio la sita la kuchoma moto nyumba za ibada kwa kipindi cha mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment