Pages

Friday, 25 September 2015

Magufuli apokelewa Kahama kwa Kishindo

Magufuli akiimba wimbo wa kampeni
na wananchi.

Wananchi wakimsikiliza mgombea

Magufuli akinadi ilani ya chama mkutanoni


Magufuli akishuka ktutoka katika gari kwa kuruka

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi "CCM"  Dr.John  Mgufuli, ameendeleza kauli ya kuwaahidi wananchi  hatowaangusha Watanzania pindi akichaguliwa kushika nafasi ya urais octoba 25.
Magufuli akiwa katika kampeni zake alisema changamoto za wilaya ya Kahama anazifahamu wakati utakapofika atazianisha fursa za kuzitatua.
Alisema anatambua ukubwa wa mji wa Kahama na kasi ya maendeleo iliyopo halingani na hadhi iliyonayo, na kuwahakikishia kuwa kulingana na ilani ya chama chake  wilaya hiyo itafikia hadhi stahili kulinagana na ukuaji wake.
 "Naomba muendelee kuniombea kama nilivyowaomba wakati wa mchakato ndani ya chama,na wakati ukifika,wana Kahama sitowaangusha,"Alisema.

No comments:

Post a Comment