Pages

Tuesday, 15 September 2015

Wasanii wa Gospel ndani ya Tamasha la Aman Oktoba 4,

TAMASHA la Amani linatarajiwa kufanyika Oktoba 4, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali wamepania kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki watakaojitokeza.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa wiki hii na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa wasanii hao wamesema kuna mambo mazuri watayafanya siku hiyo.


Baadhi ya wasanii waliotajwa kwamba watatumbuiza siku hiyo ni Sarah K, John Lissu, Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Boniface Mwaitege.


Taarifa hiyo inawakariri wasanii mbalimbali wakizungumzia tamasha hilo, huku wakitamba kwamba mambo yatakuwa mazuri.


"Nimedhamiria kuwapa mambo mazuri mashabiki wangu, najua watafurahi sana, watakaokuja hawatajuta," ni kauli ya Rose Muhando.


Naye msanii Upendo Nkone, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwa wana imani kubwa litakuwa tamasha zuri
.



No comments:

Post a Comment