Pages

Monday, 7 September 2015

Watu 17 majeruhi Mkutano wa CCM Morogoro

WATU 17 wameripotiwa kujeruhiwa katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Septemba 6, 2015.


Watu hao imeelezwa baada kumalizika mkutano wakati wanatoka nje ya uwanja walikanyagwa kutokana na msongamano mkubwa wa watu hivyo walikimbizwa hospital ili kupewa huduma ya kwanza na baadhi majeruhi wapatao saba wamerudi nyumbani baada ya kurejea hali ya kawaida.

Aidha katika baadhi ya watu waliojeruhiwa katika msongamano huo watu wawili walipoteza maisha walipofikishwa hospitali aidha walipoteza maisha ni mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42).

Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42).

No comments:

Post a Comment