Wengine wanaokusudiwa kushtakiwa ni Bodi ya Wadhamini wa CCM na Timu ya Kampeni ya CCM kwa kosa la kuiba haki miliki ya Chadema ambayo ni M4C.
Vyama vinavyounda Ukawa ni Chadema, NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (Cuf) na National League for Democracy (NLD), vinakusudia kuchukua hatua hiyo kwa madai mgombea urais wa CCM anaiga na kutumia nembo za Chadema kwenye mabango na hotuba zake za kampeni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, alisema watakwenda kufungua mashtaka hayo dhidi ya CCM, Jumatatu wiki ijayo na kwamba wanasheria wa Ukawa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kisheria.
Alisema lengo la kumshtaki Dk. Magufuli ni kwa kukiuka sheria kwa kutumia nembo za Chadema ambazo chama hicho kina hati miliki nazo.
Alizitaja nembo zinazotumiwa na Dk. Magufuli ambazo ni mali ya Chadema kuwa ni M4C (Movement For Change), ambayo imetafsiriwa kama Magufuli For Change na kauli ya Mabadiliko inayotumiwa na Ukawa ambayo imechukuliwa na mgombea wa CCM kama Mabadiliko Magufuli, Magufuli mabadiliko na kuiba sera na ahadi za ilani ya Chadema na Ukawa.
SOURCE:GAZETI LA NIPASHE.
No comments:
Post a Comment