Haya ni maswali ambayo Dr. SLAA aliulizwa na waandishi wa habari na kuyajibu baada ya kipindi cha hotuba yake kumalizika hapo jana jijini Dar es salaam..
1. Umetangaza kustaafu siasa (na kuachana na siasa za vyama) na uka kadi mbili (ya CCM na CHADEMA). Je, nazo utazirudisha!?
Majibu: Kadi ni mali yangu. (sitairudisha)... Sijawahi kufanya kazi ya CCM.
2. Umesema waliopokelewa CHADEMA wengine ni makapi. Mwaka 1995 ulihama CCM. Je, nawe ulikuwa kapi!?
Majibu: Mimi sikuwa mbunge niliyekataliwa. Sikuwa mwenzao, sikuwa mla rushwa.. Kama ni kapi pima mwenyewe.
3. Ulituambia kuwa Lowassa angekuwa ni asset (kwa CHADEMA kwa vigezo ulivyoweka wakati wa kumkaribisha, angekuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM mikoa 22 na wenyeviti wa CCM wilaya 80). Je yangetimia hayo huu chafu wa Lowassa ungefutika!?
Majibu: Nilisema nina vigezo viwili (kumkubali Lowassa), kama ni Asset ama Liability. Baada ya kujiridhisha na hayo mnafanya tathmin. Angetimiza hayo..hakufanya yote.. sina la kulalamikiwa.
4. Unaonekana kumshambulia sana Lowassa. Je, hii ni baada ya kukosa nafasi ya kugombea Urais CHADEMA?
Majibu: Nilieleza mwanzo. Slaa hajagombea urais, unakasirikaje kama hujachukua fomu? Sina ugomvi wala chuki na yeyote. Sina ugomvi na Mbowe. Mbowe ni rafiki yangu, hata nyumba ninayoishi alinisaidia. mimi ni masikini.
5. Kwa kutumia mfano wako wa kwamba ukihamisha choo na kukiweka chumbani, harufu ya choo itabaki ile ile.
Wewe uliweza kutoka CCM na kubadili CHADEMA. Je, waliotoka CCM sasa kama wewe hawawezi kuibadili CHADEMA (kufuata kanuni na taratibu)!?
Majibu: Dr SLaa hakuwa mchafu. Tatizo sio kuhama chama. Hakuna tatizo kuhama chama.
6. Unadhani nani anafaa kuwa Rais kwa uchaguzi wa Oktoba 25, 2015!?
Majibu: Nimeeleza tu taifa litakuwa na madhara gani huyu (Lowassa) akiwa Rais. Watanzania waache ushabiki ambao baadae watajuta. Sikuja kumtetea mtu... Kama utetezi wangu utakuwa wa upande fulani, sina namna nyingine ya kueleza.
No comments:
Post a Comment