Pages

Thursday, 17 September 2015

WAFUNGWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA DADA YAO.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida, imemuhukumu Mkazi wa Veta Kata ya Mandewa, Ramadhan John (20) na mdogo wake, Karim (18) kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kwa zamu mtoto wa kike wa dada yao (9).

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Joyce Minde baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa, washtakiwa hao walimbaka mtoto huyo wakati amelala chumbani kwake.

Hakimu Minde alisema adhabu hiyo kali dhidi ya washtakiwa hao itakuwa fundisho kwao na kwa vijana wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

" Upande wa mashitaka umethibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa washtakiwa wana hatia kama walivyoshitakiwa. Kitendo mlichofanya ni cha kinyama na hakivumiliki mbele ya jami, mahakama haina njia nyingine isipokuwa kuwapa adhabu ya kwenda jela maisha yenu yote yaliyobakia, " alisisitiza Hakimu Minde.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Micahel Ng'hoboko alidai kuwa Julai 30, mwaka jana, usiku katika maeneo ya Veta mjini Singida, washtakiwa hao walimbaka mjomba wao na kumsababishia maumivu makali.

Ng'hoboko alidai siku ya tukio mshtakiwa wa kwanza Ramadhan, alimsimulia mdogo wake Karim kuwa amekuwa akimbaka mjomba wao mara kwa mara wakati dada yao hayupo nyumbani. Alidai Karim alishawishika na kushiriki kumbaka mjomba wao usiku.

"Siku tukio ilipofika saa 5 usiku, washtakiwa walinyata na kuingia chumbani kwa mjomba wao na kumbaka kwa zamu, " alidai.

Ng'hoboko alidai mjomba wao alianza kupata maumivu makali na kupiga yowe kuomba msaada kwa mama yake.

Alidai mama yake aliamka baada ya kusikia yowe na kwenda chumbani kwa bintiye huyo na kushuhudia wadogo wake hao wakiwa utupu.

"Mmoja wa washtakiwa alipomuona dada yao chumbani aliruka dirishani na kutoroka, lakini alikamatwa kwa rafiki yake akiwa mtupu baada ya kufanyika msako mkali, " alidai Mwendesha Mashtaka.

Alidai baada ya mshtakiwa huyo kukamatwa aliunganishwa na mwenzake na si kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka na kuhukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia.

#Chanzo_Mwananchi

No comments:

Post a Comment