Pages

Monday, 14 March 2016

Athari za matumizi mabaya ya Simu kwa Watoto na Vijana

SIMU ni kifaa kikubwa kinachotumika katika mawasiliano zimekuwa kama sehemu ya maisha ya kila mwanadamu duniani kote.

Kifaa hiki kwa wengine wamekifanya kuwa sehemu
yao ya maisha kiasi kwamba mtu asipokuwa na simu anakuwa kama amepungukiwa na kiungo muhimu cha mwili wake.

Japokuwa simu ni chombo kizuri na cha uhakika kwa mawasiliano ya haraka, kujifunza mambo mapya, kukuza uchumi na mambo mengine ya maana lakini zina athari za mionzi inayopenya mwilini kama matokeo ya matumizi ya simu yamepekea athar kiafya zitokanazo na matumizi ya muda mrefu ya simu pamoja na athari za kijamii zinazotokana na kiafya kwa watoto na vijana walio chini ya umri wa miaka 20.

Leo hii tutajikita katik kuangalia matumizi yasiyo sahihi kwa watoto na vijana kwani kipindi hiki wazazi wamekuwa wanawapa simu watoto wao na bila kuwafundisha jinsi ya kutumia kwa kiasi simu hizo na unakuta mtoto mda mwingi ni kuchati tu wala hasomi tena.

Inashauriwa kuwa ni bora kwa vijana hawa kuepuka matumizi ya simu za mkononi au watumie mara chache sana tena kwa muda mfupi na pale inapokuwa hakuna njia mbadala ya mawasiliano.

Matumizi makubwa ya simu za mkononi yanaingilia utendaji wa ubongo wa vijana wadogo hivyo huweza kuathiri uwezo wa kufikiri sawasawa na kuwa makini lakini pia inasemekana kuwa, matumizi makubwa ya simu hizi katika umri mdogo, yanaongeza uwezekano wa kupata kansa ya damu kutokana na mionzi.

Vijana wanaotumia simu za mkononi kwa muda mrefu hukabiliwa na msongo, kukosa utulivu wa kiakili, hali ya kupata uchovu wa mwili na hali ya kutokupata usingizi vizuri.

Wengi hawazimi simu zao wanapokwenda kulala usiku na wengine hulala nazo kitandani karibu kabisa na kichwa, jambo ambalo huharibu mtiririko wa usingizi wakati akili inapohitaji kupumzika.

Jumbe na miito mingi ya wasichana huwa inahusiana na mambo ya kimapenzi ambayo huchochea akili kufikiria ngono kwa nguvu kutokana na ukweli kuwa wakati wa balehe, tamaa za ngono huwa na nguvu kubwa.
Simu zenye mtandao pia huwaingiza vijana wengi katika mtego wa kuangalia picha za ngono zinazochochea tamaa ya ngono haramu na hatarishi.

Akili za watoto, ikiwa ni pamoja na wasichana hudhurika kirahisi kwa mionzi na athari zake kuchukua muda mrefu hata baada ya matumizi ya simu kwa muda mfupi.

Mionzi ya simu hupenya katika fuvu la watoto kwa nguvu zaidi kuliko watu wazima waliokomaa,uwezo wa kiakili wa vijana ambao unatazamiwa kuwa utapungua wafikapo katika umri wa kustaafu kazi (miaka 60), hupunguzwa na mionzi ya simu. Wafikapo miaka 30 tu ya umri wao, vijana wanao tumia sana simu za mkononi, huwa sawa na wazee wa miaka 60 katika uwezo wa kiakili.

Tafiti kadhaa huonyesha vijana wenye umri wa miaka 20 wakiendesha gari huku wanaongea kwa simu uwezo wao wakiakili wa kufanya maamuzi huchelewa sawa na ule wa wazee wa miaka 70 na umakini wao hugawanyika katika kuangalia usalama na kutafakari maana ya ujumbe na jinsi ya kujibu.

pia huvuruga uwezo wa ubongo wa kufanya maamuzi kwa haraka,mara nyingi matokeo ya jambo hili huwa ni ajali za barabarani, zinazo sababisha madhara makubwa ya kiafya na ulemavu au vifo.

Upo ushahidi pia unaoonyesha kuwa kutumia simu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya kichwa na hisia ya ganzi katika ngozi ya kichwa. Mionzi ya simu za mkononi pia hupunguza uzalishwaji wa kichocheo cha melatonin mwilini ambacho ni muhimu kwa utendaji mzuri wa ubongo na kinga dhidi ya saratani ya matiti. Wasichana wanaotumia simu za mkononi kwa muda mrefu, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti na ugonjwa wa ubongo (Alzheimer's disease) mapema au baadaye sana katika kipindi chote cha maisha yao yaliyobaki. Hii inatokana na uwezo mkubwa wa seli za vijana kuitikia nguvu za mionzi.
Hali huwa mbaya zaidi kama simu inatoa mionzi zaidi ya kipimo cha SAR (Specific Absorption Rate) Wart 2/kg.

Tatizo jingine la kiafya kutokana na simu ni ugonjwa wa masikio kuunguruma muda wote (Tinnitus) hasa kwa vijana wanaosikiliza muziki kwa kutumia simu zao au kupokea miito ya simu yenye makelele.

Mzazi unashauriwa kuwa makini na mtoto wako na matumizi ya simu yake kwani usipo fanya hivyo sio rahisi mtoto huyo kutimiza ndoto zake maishani.

No comments:

Post a Comment