Pages

Monday, 21 March 2016

MISS TZ MSIMU MPYA WAZINDULIWA NA NAPE.Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amezindua rasmi msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 katika hafla ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi, Dar es Salaam. Uzinduzi huo umewakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo wakiwemo wabunifu wa mavazi, warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania miaka iliyopita na mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini.

Hizi ni picha mbalimbali katika tukio zima la miss tanzania.

No comments:

Post a Comment