Akizungumza na mwandishi wetu wa Shangwetzblog mwimbaji huyo amesema kwa sasa amekamilisha albamu yake yenye nyimbo kumi(10) na mwanzoni mwa mwezi huu ata anza kuzitangaza katika mitandao ya kijamii(social media) na wimbo atakao anza kuachia ni wimbo wa Acha Nikuimbie na baada ya hapo nyimbo nyingine pia sitahusika.
Agness alianza huduma ya uimbaji tangu akiwa mdogo anasoma shule ya msingi mwaka 1998 na akaanza rasmi uimbaji binafsi mwaka 2007;ambapo ameshawahi kuimba na kwaya nyingi kama Kalinzi Muungano(KVC)na mwaka 2003 ndipo alipojiunga na Upendo kwaya iliyopo Morogoro mjini.
Aidha amesema changamoto anazokutana nazo ni nyingi kwani alishawahi kurekodi albamu yake ya kwanza 2007 huko mwanza na haikuwa vizuri kwani producer hakurekodi sawia pia mwaka 2010 akarekodi albam nyingine Jijini Dar es salaam ambayo ilikwenda kwa jina la Tumrudie Mungu ambayo sasa iko sokoni japo nayo haijafanya vizuri sana.
Aidha Agness amesema kwa sasa amejipanga vizuri na anakuja kivungine na kazi yake mpya ikiwa amelenga kusambaza nyimbo zake zote na kuanza na wimbo wa Acha nikuimbie katika vituo vingi vya vya radio huku akiwa anaweka sawa taratibu za kurekodi video(DVD) ya album hiyo.
Hata hivyo Agness ameongeza kusema nyimbo zake zimebeba ujumbe wa neno la mungu kwani atakayepata fursa ya kusikiliza nyimbo hizo hakika atapata kitu toka kwa Bwana na atapiga hatua katika maisha ya kiroho na kimwili.
Albamu ya Tutamuona Bwana imefanyikia Mwanza na imesheheni nyimbo kama Tutamuona Bwana,Damu ya Yesu,Acha nikuimbie,Haleluya,Yesu anaweza,Nani atusaidie,Salama,Mtegemee Mungu na Aratambara.
Hata hivyo mwimbaji huyo alisisitiza kusema sasa ameamua kuihubiri injili kwa njia ya uimbaji mijini na vijijini; ndani na nje ya nchi sambamba na kutunga nyimbo za kutosha na kutengeneza video zenye viwango vya hali ya juu.
No comments:
Post a Comment