Rosemary alisema hakuwa na nia mbaya alipotoa kauli hiyo, bali aliitoa kwa bahati mbaya akimaanisha eneo jingine lililoko Kenya linaloitwa Olorgesalile.
Alifafanua kuwa matamshi hayo hayakulenga kupotosha ukweli, bali ulimi uliteleza,Katika maelezo yake aliyotoa kupitia akaunti yake ya Facebook.
"Habari za jioni. Nimekuwa nikikumbushwa kuhusu tukio lililotokea wakati nahudhuria kongamano la vijana New York, miezi saba iliyopita.
Niliteleza ulimi kwani sikumaanisha Olduvai Gorge badala yake nilitaka kumaanisha Olorgesalile;Nawapa pole Watanzania kutokana na usumbufu uliojitokeza, kaka zangu na dada zangu poleni sana na Olduvai Gorge yenu bado iko salama."alindika hivo Rosemary.
Kupitia Instagram, Mtoto wa Odinga aliandika:
I have just been reminded of an incident which occurred while attending IYLA in New York last year where I had a Freudian slip. Apparently our brothers and sisters from TZ are alarmed that I have grabbed their Olduvai Gorge. I meant to say our equally historic Olorgesaiile site in Kajiado. As I have learnt, what happens in New York doesn't stay in New York. So, what would Magufuli do? Sorry Tanzanians, your Olduvai Gorge is safe. In the spirit of one East Africa let's shake hands after all at the end of the day we are the cradle of humankind"
Tangu kutolewa kwa kauli hiyo, kumekuwa na mlolongo wa shutuma zinazoelekezwa kwa binti huyo wa Odinga huku baadhi ya Watanzania wakisaini azimio maalumu kumtaka ombe radhi ambalo waliosaini wamefikia 17,000.
Aidha kumekuwapo na mkanda wa video unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Rosemary akihutubia mkutano jijini New York huku akidai Bonde hilo lililogunduliwa mtu wa kale la Olduvai Gorge linapatikana nchini Kenya.
Mapema, Serikali ya Tanzania imesema itachukua hatua za kidiplomasia endapo ungepatikana uhakika juu ya taarifa zinazoenezwa na mitandao ya kijamii kuwa raia wa Kenya huzitaja baadhi ya tunu za Tanzania kuwa zinamilikiwa na nchi yao.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambeni alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana akisema Serikali inafanya uchunguzi juu ya taarifa hizo.
Hata hivyo, alisema hali hiyo inaonyesha ni jinsi gani nchi Tanzania inazidi kuwa maarufu kwa mazuri yake mpaka majirani wanatamani miliki zake.
No comments:
Post a Comment