Pages

Monday, 21 March 2016

Amani na Usalama Zanzibar umeimalika

Ulinzi umeimarishwa katika ukumbi ambao matokeo ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar yatatangazwa.

Mbwa wa ulinzi pia wametumika kukagua eneo hilo, ambalo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Selim Jecha Selim anatarajiwa kutumia kutangaza matokeo
.
Tume hiyo bado haijasema ni saa ngapi matokeo ya kwanza yataanza kutangazwa,Mwenyekiti huyo alitupiwa lawama nyingi na upinzani kwa kufuta matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25.

Licha ya kususia uchaguzi huu wa marejeo na kusema kuwa si halali, bado chama cha wananchi CUF kiliwekwa katika orodha ya washiriki katika zoezi hilo.

CUF Kiliuelezea uchaguzi huo kuwa ni batili huku ikiwa idadi ya waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo wa jana Jumapili ilikuwa ndogo.

Zanzibar ina jumla ya wapiga kura 503,860 waliojiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua rais. Majina yao ndiyo haya:
1 Khamis Iddi Lila ACT-W
2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA
3 Hamad Rashid Mohamed ADC
4 Said Soud Said AFP
5 Ali Khatib Ali CCK
6 Ali Mohamed Shein CCM
7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA
8 Seif Sharif Hamad CUF
9 Taibu Mussa Juma DM
10 Abdalla Kombo Khamis DP
11 Kassim Bakar Aly JAHAZI
12 Seif Ali Iddi NRA
13 Issa Mohammed Zonga SAU
14 Hafidh Hassan Suleiman TLP

No comments:

Post a Comment