Pages

Thursday, 17 March 2016

FAIDA ZA KULA MAYAI KWA AFYA YAKO.

Mwanadamu hawezi kuishi bila ya kupata mahitaji mhimu ambayo kwanza ni chakula,maradhi na mavazi hivyo leo tutangalia hitaji moja la chakula mojawapo ambacho ni mayai

Mayai ni miongoni mwa vyakula bora zaidi' kuliko vyote kwa afya ya mwanadamu kwani yamejaa viinilishe mhimu na vingi kati ya hivyo viinilishe havipatikani kirahisi katika vyakula vingi vya kisasa.

Katika makala hii tutazama baadhi ya faida zitokanzao na mtu kula mayai kama zilivyothibitishwa katika tafiti nyingi duniani.

Mayai yana virutubisho vya kutosha kwa afya ya binadamu na ni moja ya vyakula vyenye virutubisho vizuri zaidi moja pia linakuja na kalori au nishati 77, gramu 6 za protini na gramu 5 za mafuta yenye afya au mafuta safi kwa ajili ya mwili (healthy fats).
Mayai pia yana viinilishe vingine vidogo vidogo (trace nutrients) ambavyo ni mhimu kwa afya bora.
Hakika… mayai ni chakula ambacho ni karibu kimejikamilisha, mayai yana karibu kila aina ya kiinilishe mhimu tunachokihitaji kila siku.
Tafiti zadai Mayai huwa na kolesto nyingi lakini hayaathiri kolesto katika damu na Ukweli ni kuwa, yai moja tu huwa na
kolesto mg 212, ambayo ni zaidi ya nusu ya kiasi cha kolesto ambacho imependekezwa ule kwa siku ambacho ni mg 300.
Hata hivyo…ni mhimu kuelewa kuwa kolesto katika mlo huwa si lazima ipandishe kolesto ya kwenye damu,Kwa kawaida Ini peke yake huzalisha kiasi kingi cha kolesto kila siku wakati tunapokuwa tumekula mayai zaidi, Ini lenyewe huzalisha kiasi kidogo zaidi cha kolesto ili kusawazisha hiyo tofauti.
Matokeo ya ulaji wa mayai hutofautiana toka kwa mtu mmoja hadi mwingine:
. Asilimia 70 ya walaji wa mayai hawapati kabisa kuongezeka kwa kolesto .
. Asilimia 30 ya walaji wanaripotiwa kuwa wanatokewa kuongezeka kwa kolesto
Pia ulaji wa mayai faida yake nyingine huuongeza msongamano wa juu wa lipoprotini kolesteroli (Kolesto nzuri) ijulikanayo kwa
kiingereza kama 'High Density Lipoprotein' (HDL). Ambayo hujulikana kama ni kolesto nzuri, maana kuna
kolesto nzuri na kolesto mbaya.
Watu wenye msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto kwa kawaida huwa na uwezekano mdogo wa kupatwa na maradhi kama ugonjwa wa moyo, stroke na matatizo mengine mengi ya kiafya.
Kula mayai ni njia nzuri ya kuongeza msongamano wa juu wa lipoprotini
kolesto.
Katika moja ya majaribio; kula mayai 2 kwa siku kwa wiki 6 kuliwezesha kuongezeka asilimia 10 ya msongamano wa juu wa lipoprotine.
Mayai yana kiinilishe mhimu sana kiitwacho 'Choline'
Choline ndicho kiinilishe mhimu kabisa ambacho watu wanakikosa na watu wengine hawana habari kabisa juu ya uwepo wake pia kiinilishe mhimu zaidi na mara nyingi hupangwa pamoja na vitamin za kundi B.
Hiki ni kiinilishe kinachopatikana katika mayai ambacho kazi yake kuu mwilini ni kutengeneza ukuta wa seli na kinacho kazi pia kutengeneza molekuli za hisia katika ubongo na kazi zingine nyingi.
Tafiti zinaonyesha zaidi ya asilimia 90 ya watu wanapata kiasi kidogo cha choline kati ya kile ambacho kimependekezwa kila mmoja ale kwa siku.
Yai zima, lote, ni chanzo kizuri cha choline. Yai moja huwa na zaidi ya mg 100 za kiinilishe hiki mhimu ambacho watu wengi hawakijuwi.
Kadhalika Mayai yana protini yenye ubora wa hali ya juu na amino asidi mhimu kwa uwiano mzuri na Protini ndiyo matofali mhimu zaidi katika ujenzi wa mwili wa binadamu.
Protini hutumika kutengeneza aina zote za tishu na molekuli ambazo ni mhimu katika ujenzi na ufanyaji kazi wa mwili sanjali na Kupata kiasi cha kutosha cha protini katika mlo wako ni mhimu sana
utafiti waonyesha kiasi cha protini ambacho kimependekezwa kuwa ndicho unachopaswa kula kila siku chaweza kuwa ni kidogo sana.
Ndiyo… mayai ni chanzo kizuri kabisa cha protini, huku yai moja likiwa na gramu 6 za protini.
Mayai yana amino asidi zote mhimu zaidi kwa usawa mzuri na hivyo mwili wetu unakuwa umehakikishiwa utumikaji wa protini hiyo ipatikanayo katika mayai.
Kula kiasi cha kutosha cha protini kunaweza kuwa msaada katika kupunguza uzito, kuongeza uwingi wa mishipa, kupunguza shinikizo la juu la damu na kuimarisha afya ya mifupa, kwa kuyataja machache kati ya mengi ya faida ya ulaji wa kutosha wa protini.

No comments:

Post a Comment