Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge zinasema kuwa, Waziri Kigoda amefariki jana majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Appolo nchini India.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa kuhusu taratibu za msiba huo, ikiwa ni pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu na mipango yote ya mazishi zitaendelea kutolewa na Serikali pamoja na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu kadri zitakavyoendelea kupatikana.
Waziri huyo alipelekwa India kwa matibabu mapema mwezi Septemba
#Mwananchi
No comments:
Post a Comment