Pages

Wednesday, 2 March 2016

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA GOSPEL: AGNESS KUACHIA SINGLE YA ACHA NIKUIMBIE

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili toka Mwanza Agness Nkugwe anayekuja kwa kasi sana mwezi huu anaachia single ya Acha Nikuimbie ikiwa ni wimbo ulimo katika albamu yake mpya ya Tutamuona Bwana.

Akizungumza na mwandishi wetu wa Shangwetzblog mwimbaji huyo amesema kwa sasa amekamilisha albamu yake yenye nyimbo kumi(10) na mwanzoni mwa mwezi huu ata anza kuzitangaza katika mitandao ya kijamii(social media) na wimbo atakao anza kuachia ni wimbo wa Acha Nikuimbie na baada ya hapo nyimbo nyingine pia sitahusika.

Agness alianza huduma ya uimbaji tangu akiwa mdogo anasoma shule ya msingi mwaka 1998 na akaanza rasmi uimbaji binafsi mwaka 2007;ambapo ameshawahi kuimba na kwaya nyingi kama Kalinzi Muungano(KVC)na mwaka 2003 ndipo alipojiunga na Upendo kwaya iliyopo Morogoro mjini.

Aidha amesema changamoto anazokutana nazo ni nyingi kwani alishawahi kurekodi albamu yake ya kwanza 2007 huko mwanza na haikuwa vizuri kwani producer hakurekodi sawia pia mwaka 2010 akarekodi albam nyingine Jijini Dar es salaam ambayo ilikwenda kwa jina la Tumrudie Mungu ambayo sasa iko sokoni japo nayo haijafanya vizuri sana.

Aidha Agness amesema kwa sasa amejipanga vizuri na anakuja kivungine na kazi yake mpya ikiwa amelenga kusambaza nyimbo zake zote na kuanza na wimbo wa Acha nikuimbie katika vituo vingi vya vya radio huku akiwa anaweka sawa taratibu za kurekodi video(DVD) ya album hiyo.

Hata hivyo Agness ameongeza kusema nyimbo zake zimebeba ujumbe wa neno la mungu kwani atakayepata fursa ya kusikiliza nyimbo hizo hakika atapata kitu toka kwa Bwana na atapiga hatua katika maisha ya kiroho na kimwili.

Albamu ya Tutamuona Bwana imefanyikia Mwanza na imesheheni nyimbo kama Tutamuona Bwana,Damu ya Yesu,Acha nikuimbie,Haleluya,Yesu anaweza,Nani atusaidie,Salama,Mtegemee Mungu na Aratambara.

Hata hivyo mwimbaji huyo alisisitiza kusema sasa ameamua kuihubiri injili kwa njia ya uimbaji mijini na vijijini; ndani na nje ya nchi sambamba na kutunga nyimbo za kutosha na kutengeneza video zenye viwango vya hali ya juu.

UMUHIMU WA MACHUNGWA KWA AFYA

Machungwa ni miongoni mwa matunda maarufu yanayolimwa sehemu mbalimbali nchini na duniani na matunda hayo ni jamii ya matunda aina ya citrus na  inajumuisha machungwa na machenza n.k

Watu wengi wamekuwa hawana utamaduni wa kula matunda wakati mwingine sio kwa kukosa uwezo wa kuyanunua ila ni kupuzia na wengine kutokujua umhimu wake katika afya ya binadamu.

Ukiwa na utamaduni wa kula matunda hakika utakuwa mtu wa tofauti hususani machungwa kwa kuwa kuna Virutubisho ndani ya machungwa.

Kazi ya machungwa katika mwili wa binadamu ni chanzo kikubwa  cha Vitamini C katika mlo, Chungwa lenye ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na miligramu 75 kwa mwanamke.

Vitamini C iliyomo kwenye chungwa huimalisha uzalishaji wa Seli hai nyeupe zinazoimalisha kinga mwilini na unapokuwa na kinga imara huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.

Machungwa yaweza kuliwa au kutengenezea juisi, kwani juisi yake huwa na virutubisho vyote vya machungwa isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi mtu napokula chungwa zima.

Inashauriwa kula chungwa moja au mawili kwa siku, kwani hii hutosheleza mahitaji ya Vitamin mwilini.

Aidha machungwa huimarisha afya ya fizi na mdomo;Vitamini C husaidia kujenga protini za kolajeni za fizi za mdomoni, hii huimarisha afya ya fizi. Ukosefu wa Vitamini C mara nyingi huambatana na fizi kuvuja damu kutokana na kukosa protini za kolajeni za kutosha.

#Afyakwanza.

Monday, 29 February 2016

FAHAMU UTARATIBU WA UPIMAJI WA ARDHI MAENEO YA MJINI.

Tunapoongelea upimaji ifahamike kuwa upimaji upo wa aina nyingi.Kutokana na hilo upimaji unaoongelewa hapa ni upimaji miliki. Lakini pia tunaongelea upimaji miliki wa ardhi mijini na sio vijijini.

Upimaji wa ardhi miliki ni upimaji ambao lengo lake ni kummilikisha mtu ardhi. Kummilikisha mtu ardhi sio kumuuzia ardhi. Kummilikisha mtu ardhi ni kutambua ardhi yake kimipaka na kumpatia nyaraka mahsusi(specific) inayohusiana na umiliki( hati).
Kwa maana hii wanaomiliki ardhi ambazo hazijapimwa hatuwezi kusema wamemilikishwa ardhi .

Haijalishi ardhi hizo ni za kwao na wamezinunua kwa pesa zao. Kwa kusema hivyo haimaniishi kuwa ambao hawana hati au hawajapima ardhi zao basi sio wamiliki, hapana isipokuwa ni kuwa tu kwamba hawajamilikishwa kisheria na mamlaka za serikali.

Kutokana na hilo ardhi iliyopimwa na ile ambayo haikupimwa hutofautiana hadhi na thamani kwa kiasi kikubwa.

1.NYARAKA ZINAZOHITAJIKA ILI UPIMIWE ARDHI.

( a ) Barua kwenda kwa mkurugenzi. Anayetaka kupimiwa ardhi anatakiwa kuandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri husika. Barua ni nyaraka ya kwanza kabisa ambayo unatakiwa kuwa nayo. Ni katika barua hiyo ambamo utaeleza nia yako ya kutaka kupimiwa ardhi na matumizi ya ardhi yako kama ni makazi,kiwanda n.k.

( b ) Kuambatanisha mkataba wa mauziano. Katika hatua hii mkataba wa mauziano utatambuliwa kama nyaraka ya umiliki. Mkataba huu ndio utakaokutambulisha kama mmiliki wa ardhi husika. Huu unaambatanishwa kwasababu mmiliki wa ardhi ndiye mwenye jukumu la kuomba kupimiwa.
Hivyo kuambatanishwa kwa mkataba kunathibitisha kuwa mmiliki ndiye anayeomba kupimiwa kwa mujibu wa sheria. Ni vema mkataba wa umiliki ukawa ni ule mkataba wa kisheria ulioandaliwa na kushuhudiwa na mwanasheria.

( c ) Barua iliyotajwa hapo juu katika "A" hakikisha ina muhuri wa mwen yekiti wa serikali za mtaa, sahihi pamoja na mhuri wa mtendaji. Mwenyekiti na mtendaji atakayetumika sio wa pale unapoishi bali pale lilipo eneo unalotaka kupima. Kama eneo lipo unapoishi basi utamtumia huyohuyo wa eneo unaloishi.

2. HATUA ZA KUPIMIWA.
Hatua hizi ni muhimu kuzifahamu kwakuwa unapokuwa katika mchakato huu unahitaji sana kujua kazi yako imekwama wapi na kwa nani ili kama kulalamika ujue pa kuanzia. Wanaofanya kazi za ardhi watajua namaanisha nini.

( a ) Barua niliyotaja hapo juu itawasilishwa kwa mkurugenzi wa manispaa . Barua hiyo itakuwa imeambatanishwa na nyaraka nilizotaja hapo juu. Manispaa inayotumika siyo ile unayoishi bali ni ile lilipo eneo husika.

( b ) Baada ya barua hiyo kufika kwa mkurugenzi basi huwasilishwa kitengo cha ardhi. Kila manispaa ina kitengo cha ardhi. Hapo hushughulikiwa na afisa ardhi ambae kazi yake kubwa itakuwa ni kuthibitisha uhalali wa umiliki wa mwombaji.

( c ) Ikitoka hapo kwa afisa ardhi inaenda mipango miji. Afisa ardhi huipeleka kwa afisa mipango miji kwa fomu ijulikanayo kama SF 47. Kazi kubwa ya afisa mipango miji ni kutizama iwapo eneo linaloombwa kupimwa lipo katika ramani ya mipango miji.Kama limo katika ramani basi ataangalia matumizi aliyoomba mwombaji kama yanafanana na yaliyoainishwa katika ramani walizonazo.

( d ) Afisa mipango miji akishathibitisha na kuhakiki basi atatuma fomu maalum SF 47 kwa afisa ardhi mteule. Huyu kazi yake ni kujaza fomu maalum SF 37 ambayo ni ya maombi ya kupimiwa ambayo ataiwasilisha kwa afisa upimaji. Atafanya hivyo kwa kuambatanisha ramani husika.

( e ) Mwisho mpima ardhi atatoa maelekezo kwa mpimaji mahsusi ambaye ndiye sasa atafanya kazi ya kuja kufanya vipimo na utapimiwa ardhi kwa ajili ya usalama na kuipandisha thamani ardhi yako.
Haya yote yatafanyika kwa kufuata sheria namba 4 ya ardhi na kanuni zake .
Mwandishi wa makala hii ni Mwanasheria na Mshauri wa Sheria kupitia Gazeti la Serikali la Habari Leo.
#Copy:Michuzi blog.

Magazeti ya leo Jumanne March 1,2016