Mlemavu wa macho
Je, yeye anaona nini haswa?
Watu hudhani kwamba watu waliopofuka huona weusi tititi,lakini kulingana na uzoefu wa mwandishi huyu hilo si kweli.
Anasema kwamba kila anapoulizwa ni nini haswa anachokikosa kwa kuwa yeye ni kipofu husema ni giza.
Huo ndio mwanga waonao vipofu
''Unapoingia katika matandiko huwezi kuona kitu kabisa.Unapofunga macho kila kitu kinabadilika na kuwa giza''.
''Kwa hivyo upofu ni sawa na giza?
Inaingia maanani lakini si kweli''.
''Ijapokuwa uhusiano wangu wa akili na macho umekatika duniani haijawa giza kwangu.
''.Kwa hivyo unapopofuka ni nini haswa unachoona? aliulizwa
mwandishi huyu. ,''jibu ni mwangaza,mwangaza mwingi sana ,rangi za
kung'ara,rangi nyingi zinazobadilika kila mara na mwangaza mbaya ulio na bughudha''.
No comments:
Post a Comment