Pages

Wednesday, 24 August 2016

SHANGWETZBLOG TUNAWAPA POLE WAFIWA.


Blog ya SHANGWETZ tuna toa pole kwa ndugu jamaa na marafiki kufuatia na tukio la kinyama la majambazi  kuwauwa polisi wanne usiku wa kuamkia leo  baada ya kuvamia tawi la Bank ya CRDB lililopo Mbande Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Mungu awape wepesi na awe faraja kwenu wafiwa.

MUNGU BARIKI JESHI  NA TANZANIA YETU.

MAJAMBAZI YAUA POLISI WANNE DAR.





Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekamatwa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.

Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.


Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.

Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.

“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.

Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.

Monday, 22 August 2016

Mtu mmoja ameza visu 40 nchini India

MTU  mmoja nchini India afanyiwa upasuaji  kuondoa visu tumboni ambavyo amelivimeza ndani ya miezi miwili na kufikia visu 40.

Kwa mujibu wa daktari ambaye aliongoza operesheni alisema inasemekana mgojwa huyo kumeza visu ilikuwa ni tabia yake sugu kwa kuwa alikuwa anameza visu hivyo kwa siri bila hata familia yake kujua,

Hata sisi Madaktari tuliobobea katika fani hii tulipata changamoto katika kufanya upasuaji huo "Dk.Jatinder Malhotra aliiambia CNN.

Dr.Malhotra alisema mgojwa huyo mwanamme mwenye umri wa miaka 42 aliwashukuru madaktari kunusuru maisha yake pia aliomba msamaha familia yake.



Lakini swali kubwa aliloulizwa "kwa nini  kuanza kula visu? "Hata mimi sijui ni kwa nini Nilikuwa nakula visu, Lakini ilikuwa starehe nilipenda ladha yake nikawa addicted(muhanga) ... kama jinsi watu wanavyokuwa addicted na pombe na mambo mengine, hali yangu ilikuwa ni sawa" mgonjwa aliiambia CNN.