Monday, 24 July 2017
DENI LA UPENDO♡
❤Kila mtu anataka kupendwa, kupendwa raha Sana,!!
😃 hata mimi ninapenda kupendwa!🏃🏾
💕Kupendwa kuliko endelevu! Upendo wa juzi na jana na kesho na kesho kutwa uendelee kuongezeka na kuwa mkubwa zaidi na zaidi.
💓Haijalishi ni wakati wa mchana ama usiku, masika ama kiangazi, una pesa au huna pesa, yaani Nyakati zote na hali zote ninadai kupendwa!
🙈Lakini ni nani huyu anayelipa Hii gharama ya kupenda? Kwa mazingira gani atakaa amalize kulipa deni hili la kupenda?
🤝Kama vile mimi ninadai kulipiwa deni langu la kupendwa kadhalika nami natakiwa nilipe deni la kumpenda mtu!
🙌🏾Kama vile ninavyohitaji upendo wa Mama kadhalika Mama anahitaji upendo wangu kwake!
🙆🏾♂Mama yangu ana deni kwangu na mimi nina deni kwake!
😳😳😳Jirani,ndugu,jamaa na marafiki nawadai kupendwa na Kwa kipimo kilekile ama zaidi nina Deni kubwa la kuwapenda!
🙆🏾♂Lipo deni ninalodaiwa hata sasa! Nawezaje kulilipa lote likaisha? "Nikishalipa mimi, ndipo nitalipwa ninachodai "
*DENI LA KUPENDA!*
Deni hili halitakaa liishe, Na Kwa kiasi tunacholipa bado halijaisha.
❤Ni kiini cha imani YA Mkristo. Twalipa kila siku bado lingalipo deni la kupenda!
💑Kwa wanandoa kama itafika siku ukafanikiwa kulipa Deni lako lote, ujue ndio mwisho wa ndoa yenu!
Ili dunia iwe kitovu cha amani ni kila mtu kujitahidi kulipa deni lake kwa watu wote!
🤔Wakristo wanalo deni la kuwapenda wakristo wenzao kwa sababu wameunganika nao katika Kristo na kuwa mwili mmoja na kushirikiana kama familia ya Mungu.
💕Pendo lasitiri wingi wa dhambi! Kwa sababu usiyopenda kutendewa huwezi kumtendea mtu mwingine!
🕺🏾Na kila mtu huvuna alichokipanda hivyo kutamani kuvuna mazao mazuri maradufu ya vile alivyopanda!
❤Amri kuu ni hizi :Kumpenda Mungu Na kumpenda jirani yangu Kama nafsi Yangu.
💓Pendo lapenya ndani ya maneno ya sheria na kuvifunua viini vyake na kuonesha nia na shabaha ya sheria ambayo inazidi yaliyotajwa katika sheria hiyo. Kama sheria imesema nisiue, pendo hutazama ndani zaidi na kuona chuki ndani ya moyo ni dalili za uuaji!
👉🏾Hutizama na kuona masengenyo, uongo ni misumari ya moto inayojeruhi kiasi cha kuua nafsi ya Mtu! Kusamehe ni sehemu ya kulipa deni hili. Kana unabisha Mungu anasema Yeye pia hatalipa Deni hili kwako.!
🙆🏾♂Tuna Deni kubwa sana la kulipa,mkopo wa benk hauwezi kulipa deni hili! Ukiuza vyote ulivyo navyo huwezi kumaliza kulipa deni Hili.
🙏🏾Ashukuriwe Mungu aliyefanya kanuni hii maana hata matajiri wakubwa kabisa na Kwa wadogo hawajaweza kulipa deni hili. Sote tunadaiwa!
🤣😃😀Leo nimekumbuka kuwa wasomaji wangu mnanidai deni la kuwapenda! Japo na mimi pia nawadai!
🙈 Yaani tunadaiana!! Nina jaribu kulipa kwa kusema haya ili tuendelee kulipana.!
🏃🏾Tenda Wema nenda zako,unavyotaka kungojea shukrani, 😳kwani umemaliza deni lako ? Waswahili wakawavunja moyo Wale wanaofikiri eti wamemaliza madeni yao! "shukrani ya punda ni...... "malizia mwenyewe!
👊🏽Ila tutiane moyo ili kila mtu ajitahidi kulipa deni Lake kwa wakati! 😥Ukichelewa sana kulipa deni lako mali zako zitapigwa mnada ili kulipa deni hili. Mfano mtu kususiwa kwenye msiba,sherehe ni ili ajifunze kwamba 💸pesa Peke yake haitoshi kulipa deni la kupenda!
❤❤❤❤
©Dennis Ngowi
"Natazamia mbingu mpya na nchi mpya "
Sunday, 23 July 2017
Thursday, 20 July 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)