Pages

Wednesday, 8 October 2014

Picha za Halima Mdee akirudishwa Gereza la Segerea.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee  alikosa dhamana na kupelekwa rumande katika Gereza la Segerea.
Mdee pamoja na wenzake wanane, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko usio halali.

Mdee akitoka ndani ya Makakama na kusalimia raia


Halima Mdee (Mwenye suti nyeusi) na wafuasi wengine wa Chadema  wakisindikizwa kupanda gari la polisi baada ya kutokamilika kwa dhamana yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Dar es salaam.
Mdee akiongea na wana habari akiwa ndani ya gari

Mhe, Said Hassan Said sasa ndie Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar baada ya kupigwa chini Mhe, Othman Masoud Othman

Mhe, Othman Masoud Othman

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55(1)cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.

Uhuru Kenyatta afikishwa Mahakama ya ICC

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wa upande wa kulia
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.
Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.
Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.
Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.

Mtu wa kwanza aliyeugua ugonjwa wa Ebola nchini Marekani amefariki




Mtu wa kwanza aliyeugua  ugonjwa wa Ebola nchini Marekani amefariki ,hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa afya katika hospitali ya Texas.
Thomas Eric Duncan mwenye picha hapo juu aliambukizwa Ebola  huko nchini Liberia ,alikuwa amewekwa katika karantini katika hospitali moja ya mjini Dallas ili kupewa dawa za majaribio.
Awali ,Marekani ilitangaza masharti mapya ya usalama katika viingilio vyote vya taifa hilo ili kuwakagua wasafiri walio na dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3000 wamefariki na wengine 7500 kuambukizwa wengi wao kutoka Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Ebola.
Huku Dancun akiwa raia wa kwanza nchini Marekani kupatikana na ugonjwa huo,raia watatu wa Marekani pamoja na mpiga picha mmoja waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo nchini Liberia.
Habari hizo zilijiri mda mchache tu baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry kutoa wito kwa mataifa yote kuimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugonjwa huo.

Wednesday, 1 October 2014

Mwanausalama wa Obama kaacha kazi


 
Mkuu wa Idara ya Usalama nchini Marekani, aliyekuwa na jukumu la kumlinda Rais Barack Obama, amejiuzulu kufuatia matukio yenye kuhatarisha usalama wa taifa yaliyotokea.
Mkuu huyo wa usalama Julia Pierson alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Jumatano.

Siku moja kabla, alikabiliana na maswali ya wajumbe wenye hasira kutoka Baraza la Congress juu ya udhaifu mkubwa wa usalama wa Ikulu ya Marekani

Habari za tukio lingine likimhusisha mtu mwenye silaha kuruhusiwa kuingia katika lifti moja na Bwana Obama kulizidisha kutolewa wito wa kumtaka mkuu wa usalama kujiuzulu.
"Leo, Julia Pierson, mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Marekani, amenikabidhi barua ya kujiuzulu, na nimeikubali," Waziri wa Usalama wa Taifa Jeh Johnson aliandika katika taarifa.
"Nampongeza kwa utumishi wake wa miaka 30 katika idara ya usalama na taifa."