Mhe, Othman Masoud Othman
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi
Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55(1)cha Katiba
ya Zanzibar ya 1984.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe,
Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza
leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa
mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984
na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment