Pages

Monday, 5 January 2015

Siku 3 za miujiza DCT

Kanisa la Dar Calvary Temple limeandaa mkutano mkubwa wa  siku tatu utakao ambatana na ishara na miujiza katika kanisa hilo lililopo Tabata shule jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika ibada hapo  jana mchungaji kiongozi wa kanisa Ron Swai ambaye ni Katibu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God(TAG)alisema wameandaa mkutano huo kwa lengo la kuwafikishia injili wakazi wote wa jiji hili la Dar es Salaamu ambapo mnenaji ni Mwinjilisti wa Kimataifa Johannes Amritzer toka Sweden.
Mchungaji Swai alisema watu wenye wagojwa na shida mbalimbali wajitokeze kupokea muujiza wao mwaka huu mpya 2015 ''kwa sasa maandalizi yamekamilika na mnenaji Johannes atawasili Dar es Salaam hivi karibuni  kwaajili yakuitenda kazi ya Bwana''
Aidha mkutano huo utaanza Ijumaa tarehe 9 hadi 11mwezi huu mda ikiwa saa 4:30 hadi saa 12:00 Jioni na jumapili saa 7:00-3:00 asubuhi na saa 4:00-6:30 mchana.
Mchungaji alisema katika mkutano huo utakao fanyikia ndani ya kanisa utahusisha Sifa na Kuabudu  ambapo  praise and worship team wa DCT  wataongoza ibaada  ya  sifa  na kuabudu na upande wa waimbaji  watakao kuwepo kuhudumu ni Ambwene Mwasongwe,Samuel Mtasha,Victor Aron,Paul Clement na Atosha Kisava.

No comments:

Post a Comment