Pages

Monday, 2 May 2016

JE WAJUA FAIDA YA KUNYWA JUISE YA MIWA KWA KIAFYA?

Miwa ni zao linalolimwa kwa baadhi ya mikoa hapa nchini na limekuwa chanzo cha kuinua maendeleo ya kiuchumi baina ya mtu mmoja na Taifa kwa ujumla wake. Zao hilo limekuwa na umaarufu sana kwan kila binadamu analitegemea kwa lengo la kumpatia virutubisho mwilini, ikiwa ni chanzo kikubwa sana kuweka sukari mwilini sambamba na kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo
Miwa hutumiwa na wafanya biashara sana hususani katika Jiji la Dar huuza miwa ikiwa kama njugu mawe alafu imekatwakatwa katika vipandevipande kutengeneza juise kwakukamua na mashine na kupata kimiminika cha maji ya miwa ambayo hunywewa kama juise. Kwa mujibu wa wataalam wa afya wanasema kuwa kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11 zamadini halisi: na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.
Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa. Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Faida kubwa ipatikanayo kwa kunywa juise ya niwa ni kupata Virutubisho vilivyopo kwani vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi. Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukari yake ni halisia

No comments:

Post a Comment