Pages

Tuesday, 17 May 2016

WCF NA ILO WATOA MAFUNZO WA MADAKTARI













MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanza kutoa mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. 

Katika mafunzo hayo wataweza kuwafikia  madaktari wapatao 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo hayo.

Aidha mafunzo yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya na wataalamu wawili kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi ndiowatakaofundisha ambaoni Dr. Jacques Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.

 Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa kutokana na kazi.

 Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha, Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki. Bw. Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata ajali au kuugua na wakapata ulemavu”


Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu

No comments:

Post a Comment