Kikwete: Naendelea kuimarika kila siku japo sipo fit kabisa. Leo nazungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa, umeenda vizuri ukiacha maeneo machache. Ni uthibibitisho wa kuendelea na kukomaa kwa demokrasia na natoa pongezi kwa walioshinda na wakae chini kupanga mikakati ya kuongoza maeneo yao. Katika taarifa ya waziri Ghasia alielezea kasoro zilizojitokeza na aliahidi kuchukua hatua. Nieleze furaha yangu kwa Hawa Ghasia juu ya hatua alizochukua na mimi nikaweka ridhaa yangu, lazima watumishi wajue kuna adhabu ya makosa wanayoyafanya, kuwawajibisha itakua fundisho kwao na kwa wengine wawe makini kwenye uchaguzi wa 2015.
Jambo la pili ni sakata la Tegeta escrow, wakati wa bunge la bajeti kulitokea madai kuwa fedha za escrow zilizokuwa benki kuu zimechotwa kinyemela na PAP kwa kushirikiana na viongozi wa serikali. Serikali iliahidi kutekeleza kwa kupitia kwa CAG kufanya ukaguzi ambayo ilisomwa bungeni pia niliagiza kuchapishwa kwenye magazeti na tovuti ya serikali, TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi wao, taarifa yao ni kuwaona mahakamani, hawana ya maelezo. Tarehe 8 Desemba nilipoanza kazi, niliyasoma na kutoa maagizo, zipo taarifa nilizozipata japo sio zote, lakini nilisema siwezi kusubiri sana. Katika kusoma makaratasi na kupewa maelekezo, yapo mambo manne mikataba ya umeme, umiliki wa PAP, kodi ya serikali na tuhuma za rushwa.
Mikataba ya kununua umeme unaozalishwa na makampuni binafsi, mikataba ya umeme iko ya namna mbili tozo ya umeme ikiwa ni malipo ya umeme uliotumiwa kulingana na bei waliyokubaliana na ya pili ni gharama ya uwekezaji(capacty charge) kwa Songas, Aggreko, IPTL
Anaelezea historia ya mgogoro wa TANESCO na IPTL, TANESCO na IPTL walikubaliana kuanzisha akaunti ya Tegeta escrow benki kuu na kuingia mkataba, wizara ya madini kwa niaba ya TANESCO na IPTL na benki kuu kama wakala. Masharti ilikua kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake TANESCO ya tozo ya uwekezaji na TANESCO itaendelea kulipa lakini yataenda escrow akaunti badala ya IPTL lakini ya umeme yaliendelea kwenda IPTL na ilifunguliwa 2006 na mpaka kesi kuamuliwa 2013 wakati IPTL inachukuliwa na PAP walikua hawajamalizana. (They decided to manage the crisis rather than resolve it)
Kwa mujibu wa mkataba, TANESCO isipolipa inatozwa riba ya 2%, kwa mujibu wa taarifa akaunti ilikua na 202.9 bilioni na sio 309.7, hizi zilipaswa kuwepo endapo TANESCO ingelipa zote kwa wakati.
Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.
Akaunti ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji, zinahifadhiwa ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao lakini kabla ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.
Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, mdhibiti wa hesabu alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL, Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.
Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo kupunguzwa, kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima zirudi kwa kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae halikuwa limefanyika.
Kama katika fedha hizo ipo kodi ya serikali, kwa mujibu kulikua na kodi ya ongezeko la thamani ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikua bilioni 21 na ushee, TRA imepeleka madai yake kwa PAP.
CAG aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu pesa walizolipa kwenye akaunti ya escrow kama pesa zao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya TANESCO(Asset). Mahakama kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na mahakama ikakubali.
Mfilisi aliagizwa kuhamisha kwa PAP kutoka IPTL ikiwemo akaunti escrow, ilizua mjadala mkali. Wizara ya nishati ilimwandikia mwanasheria mkuu kuomba ushauri, Mwanasheria akasema lipeni, uamuzi uko sawa na hauna matatizo na benki kuu wakauliza maswali hayo hayo na majibu yakawa yaleyale. Kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa PAP. Mjadala ukaendelea bunguni na kwenye mablogu.
Na hata TANESCO alipewa ushauri huo huo, uamuzi ule umetiliwa shaka na kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu kunufaika binafsi. Mara kuna watu wameenda benki na kubeba pesa kwenye sandarusi, lumbesa na mengineyo.
Jambo moja ambalo ni bahati mbaya, ilijengeka dhana kuwa akaunti kufungwa ni jambo lililoanzishwa na maafisa wa serikali kwa manufaa yao binafsi.
Nilipokutana na mwanasheria mkuu, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala mahakama haikufanya makosa,
Na kuhusu ile hasara amesema hakuna hasara yyte iliyopatikana kwa sababu pesa imelipwa kwa mtu halali.
Kabla ya mzozo wa ukokotoaji TANESCO ilikuwa inailipa ITPL Moja kwa moja. Lakini hata ulipotokea mzozo bado IPTL haikuacha kupeleka madai na Tanesco haikuacha kulipa. Kuwepo kwa akaunti ya escrow haibadili mwenye fedha yake.
Kwa upande wa kodi ya serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa.
Mgogoro ni baina ya IPTL na TANESCO havyo uamuzi wa standard charted haukuweza kuingia, kwa vile haikuhusishwa, ilienda kuzuia maamuzi hayo.
Fedha zilizotoka imelipwa PAP, akitokea mtu ana madai, serikali mnaikinga vipi. Ingetokea mtu ana madai yoyote angepelekwa PAP kulingana na makubaliano. Kukawa kuna hoja kuwa hata PAP umiliki wake wa hisa 70% unatia mashaka kutoka Mechmar, lakini waliziuza kwanza kwa kampuni ya Uingereza ambayo yenyewe ndo ikaziuza PAP. Kampuni ilikua chini ya ufilisi na kwa mujibu wa taratibu huwezi kuuza ukiwa chini ya ufilisi, kwa mujibu wa taarifa sio kweli.
Tulitaka kufanya uchunguzi sisi wenyewe na mamlaka zetu na taarifa zimeshakuja, tunazifanyia kazi.
Kuna vitu vimetokea, kuna vilivyofanyika nje na taarifa hazikuja na sasa tunalaumiana, hivyo tunafanya uchunguzi na wote waliohusuka tunawahoji na mahakama kuu ipo kesi ya PAP kumiliki hisa za IPTL, ipo kesi ya uhalali wa PAP kupokea pesa za IPTL. Hatutaki kuwaingilia ila sisi tutafanya uchunguzi wetu kwa ajili ya taarifa zetu. Tuwe na uhakika hizi hisa zimeuzwa kwa bei gani, tunataka kujiridhisha kwa sababu ipo kodi ya serikali(capital gain) na inalipwa na alieuza na sio alieuziwa. Kodi hulipwa na aliepata na sio aliepoteza(Alienunua).
VIP walipouza na kupata dola milioni 78, wamelipa kodi bilioni 38. Kulikua na tuhuma za rushwa katika mchakato mzima. Yamesemwa mengi na bado hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa walizozipata wazipeleke PCCB. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao. Kwa miamala, serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa taratibu, maaskofu na masheikh kupewa kitu hawatuhusu, mtumishi wa umma ana masharti ya kupokea fedha. Watahojiwa na PCCB.
Hushtuki asubuhi akaunti ina bilioni 1.6, milioni 80 etc. Zimeanguka kutoka juu ya mti. Huo ndo utanguliza.
Maazimio ya bunge
Kwanza niseme serikali imayakubali na niwapongeze waheshimiwa wabunge. Nashukuru kamati ya bunge chini ya Zitto na Filikunjombe, watu wa upinzani kufanya yale maamuzi yao, kwamba CCM ni mafisadi. Ni kweli watu hawa wanatoka CCM ila sio kwamba CCM inaridhia. Ntashangaa mbunge kulipinga hili eti kisa tu yuko CCM, bunge wengi ni CCM, kama ni kweli walikuwa hawataki hakuna azimio lingepita? Na kuna baadhi ya wabunge wa CCM waliudhika na maovu haya, wenzetu wanatafuta sifa laini kwa jambo ambalo ni letu sote.
Niwahakikishie mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira katika kutimiza maazimio ya bunge.
Kutaifisha mitambo ya IPTL, tunahimiza sekta binafsi kuwekeza, tunapotaifisha habari tunayopeleka si nzuri, sisi tuliotaifisha mwanzo siku hizi tunasema hatuna sera ya ujamaa hivyo waje kuwekeza. Watasema wale jamaa wamerudia tena wanataifisha. Mahakama imefanya maamuzi kwa IPTL, kwanza waibadili mitambo yao ibadili itumie gas badala ya mafuta, tukiyafatilia yanaweza kutufikisha mahali. Haya ya kutaifisha yananipa wasiwasi
Kuhusu uwazi wa mikataba na mapitio, tutafanya na lipo moja tutafanya kuhusu usiri wao wa biashara, kuweka wazi zinaweza kutumiwa na wapinzani wa kibiashara, hivyo tutaangalia namna ya kulifanya.
TAKUKURU na jeshi la usalama vichukue hatua, nimeshaeleza hatua zinaendelea.
Kamati za bunge kuwavua nyadhifa wenyeviti wa kamati za bunge
Raisi aunde tume ya kijaji kuwachunguza majaji(Mujulizi na Lwangisa), nimelipokea lakini utaratibu wa kisheria kushughulikia linatakiwa lianzie kwenye mahakama na sio linaanzia kwa rais au bunge. Mahakama inaporidhika amepoteza sifa, inaletwa kwa rais maana ndie anaeteua majaji. Lazima kushirikiana na muhumili wenyewe. Nilichosema tumwachie jaji mkuu na wakiridhika watakuja kwa raisi endapo wataridhika wahusika wamekosa sifa.
Kuhusu mabenki kuwekwa kama zinatakatisha fedha, pendekezo uchunguzi ufanyike ni pendekezo zuri na intelligence unit ndio watakaofatilia
Serikali iandae muswada wa sheria ulioleta TAKUKURU, ni wazo zuri, Mchakato wa kufanya mageuzi TAKUKURU tumeuanza tangu 2008. Sheria ya kwanza ya PCCB ilikua na makosa manne tu ya rushwa tukayaongeza mpaka 24.
Kuhusu watu kuwawajibisha, bodi ya TANESCO bahati nzuri imemaliza muda wake na tumeanza mchakato wa bodi, na tutaipata siku chache zijazo.
Katibu mkuu wa wizara ni mtumishi wa umma, hivyo kuna taratibu na nimeshaagiza zianze.
Mwanasheria mkuu wa serikali ameshajiuzulu na amesema amebeba dhamana hio pia kwa niaba ya waliojiuzulu.
Waziri wa ardhi, tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa,tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.
Waziri wa nishati na madini tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
NDIO MWANZO NA MWISHO WA HOTUBA YANGU NDEFU
No comments:
Post a Comment