Rais Dkt Jakaya Kikwete amkaribisha Ikulu msanii wa mziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama"Diamond" nakuwapongeza na Idris Sultan mshindi wa Big brother Africa kwa kuletea sifa Taifa letu mwaka huu 2014.
Rais alimpongeza Diamond kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu 2014 alipokaribishwa Ikulu na kwa na mazungumzo na Naseeb.
Katika hatua hiyo Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul "Diamond" wakati akionyesha tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu 2014 sambamba na kumuelezea jinsi alivyoshinda tuzo hizo.
Baada ya kuongea nae kwa mda Diamond alimkabidhi Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete CD mpya ya wimbo wake unaotamba kwa sasa.
Hizi ni miongoni mwa picha 6 Jk akiwa na Diamond.
No comments:
Post a Comment