Pages

Sunday, 30 August 2015

Daktari Bingwa toka Tanzania atwaa Tuzo Uingereza.

Daktari Bigwa mshauri wa maradhi ya Moyo Dr.Harun Elmada Nyangori kutoka Hospitali ya Rufaa Morogoro hapa nchini awa mtanzania wa kwanza kupewa tuzo ya kimataifa na kutambuliwa na Baraza la Madaktari Bingwa wa Shirikisho la nchi za Ulaya (uropean Society of Cardiology).

Akitoa tuzo hiyo ya heshima kwa Dr.Nyangori Rais wa shirika hilo prof. Pinto alisema Tanzania imekuwa nchi ya pekee kuweka historia kushiriki katika mashindano ya kutoa mada za utafiti wa maradhi ya moyo.
Hivyo Dr . Nyagori amekuwa Daktari wa kwanza kushiriki na kuwa chachu ya kufungua mlango kwa madaktari wengine wajitokeze kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu taaluma ya magojwa ya Moyo.

Saturday, 29 August 2015

PICHA MATATA ZA UKAWA DAR

Ni picha matata katika uzinduzi wa kampeni za kunadi ilani na mgombea wa ukawa mh. Edward Lowassa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA eneo la jangwani jijini Dar es salaam.

Lowassa- Nitamtoa Jela Babu Seya

Katika hali isiyo ya kawaida katika mkutano wa UKAWA kupitia mgombea wake wa uraisi kupitia Chadema mh. Edward Lowassa ametoa ahadi kwa watanzania kuwa miongoni mwa vitu atakavyo vitolea maamuzi iwapo wakimpa nafasi ya kuiongoza nchi, atawatoa gerezani baadhi ya wafungwa na wawe huru.
Mh. Lowassa aliongea hayo katika ufunguzi wa kampeni za ukawa jijini Dar es salaam viwanja vya jangwani.
Lowassa baada ya kutaja ilani za ukawa alimalizia kwa kusema atahakikisha anamtoa gerezani Babu Seya pamoja na mashekhe ambao wamefugwa gerezani.
Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na mtoto wake walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto mwaka 2010.
Katika kesi yao Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana nahatia walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kuwa mwanamuziki huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa baada ya kukata rufaa kwa ombi lake la mwisho.



Baadhi ya Vipaumbele vya ilani ya UKAWA viko hapa.

Mkutano mkubwa wa uzinduzi wa ufunguzi wa kampeni za vyama vya upinzani umoja wa katiba (UKAWA)umevunja rekodi kwa kuwa kukusanya maelfu ya wanachama toka pande zote za nchi katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam..
Katika mkutano huo ukawa wamezindua ilani ya kampeni zao ambapo mh. Edward Lowassa ambae ni mgombea urais wa ukawa alipo pewa nafasi ya kuhutubia amesema wantanzania wampigie kura ili afanye mabadiliko.
Lowassa ametaja baadhi ya vipaumbele katika ila ya ukawa watafanya mabadiliko katika elimu kwa kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.
Kwa upande wa afya ukawa watatoa kipaumbele katika afya ya mama na watoto kwa kuwa ndio wahanga wakubwa katika sekita hii na mama ndio msingi wa taifa lolote duniani kwani kila mtu kazaliwa na mwanamke.
Amemalizia kwa kusema atahakikisha sekita ya usafiri inaboreshwa kwa kufufua usafiri wa ndege hususani ikiwa ni kuifufua Air tanzania.
Aidha kwa upande mwingine mh. Lowassa amemalizia kwa kuahidi wananchi wakimchagua na akawa raisi atawatoa jera mashehe na watu wengine waliopo gerezani ikiwa ni pamoja na mwanamuziki mashuri hapa nchi Babu Seya.



Wednesday, 26 August 2015

Ujue Ugojwa Hatari wa Kipindupindu.

Kipindupindu ni ugonjwa hatari wa mlipuko unaosababishwa na bakteria ajulikanaye vibrio cholera hushambulia mwilini hasa katika utumbo mwembamba baada ya hapo mgojwa huanza kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia mchele pamoja na kutapika na homa kali.

Kiwango cha kutapika sana kinaleta upungufu wa maji mwilini na kupelekea kutokuwepo na uwiano wa chumvi mwilini na huweza kupelekea mgojwa kufariki iwapo atacheleweshwa kupatiwa tiba.

Kipindupindu hutokea iwapo mgonjwa akitumia maji yasiyo safi na salama kwa kunywa.

Bakteria anayesabisha kipindupindu (vibrio cholerae) hupatikana hasa katika maji yaliyochanyika na kinyesi cha binadami na maji ya chooni.

Inashauriwa ili kujikinga kutopata maambikizi ya ugonjwa huu ni kuhakikisha unakunywa maji safi na salama yaliyochemushwa na wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula,kusafisha vyombo kama sahani,vikombe.
 unaponawa mikono hakikisha unanawa na sabuni kiganjani upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde.Baada ya kutoka chooni na kabla ya kula chakula na matunda kusafishwa vizuri na maji yaliyochemshwa.

Mgonjwa wa kipindupindu huweza kupatiwa matibabu huku lengo kuu likiwa ni kurejesha maji na madini mwilini aliyoyatoa kwa njia ya kuhara au kutapika.
Njia itumikayo kumpatia maji hayo ni kwanjia ya mdomo ambapo hupewa anywe au kwanjia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu hujulikana kama intravenously(i.v),Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya kwa njia ya kuhara na kutapika na Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.

Kura yako moja ithamini chagua kiongozi makini

Mtanzania ni siku chache zimebaki kufikia october  tutapiga kura kuchagua viongozi watakao shika madaraka ya kuongoza  taifa hili la Tanzania lenye kusifiwa duniani kwa kudumisha amani na utulivu.

Lakini pamoja na hayo leo nimekuja na swali dogo la msingi sana"JE UNATAKA KUWA NA TANZANIA YA NAMNA GANI 2015-2020?"bila shaka jiulize swali hilo kisha jijibu mwenyewe,tunapoelekea katika uchaguzi mkuu ni wakati tunapaswa kuwa makini sana kwenye kampeni za wanasiasa  wanavyo nadi ilani za vyama vyao kwetu wananchi inapaswa tufuatilie kwa umakini kwa lengo la kujue ni nini lilichomo humo.


Nasema hivyo kwasababu kampeni za mwaka huu zimekuwa za ushindani sana na wananchi wako mstali wa mbele katika ufuatiliaji na baadhi yao wamekuwa na mitazamo tofauti inayo ashiria wanajua yupi kiongozi bora hata ukiachana  na ilani za vyama husika.

Hivyo mtanzania mwenzangu hatima ya taifa letu iko mikononi mwako,namanisha sasa hivi ni mda wa kutafakari kwa umakini na kuchuja sera za wagombea ili kujua nani ni nani atafaa kupigiwa kura October.

Kura yako moja ni bidhaa hadimu tunza kadi yako na mwisho wa siku inatakiwa umpigie kura mgombea ambaye utakuwa umeridhishwa naye na kuona anafaa kusimamia rasilimali za nchi hii zikawanufaisha watanzania wote.

Mwananchi amka kura yako moja inauthamani mkubwa sana kwani ndio inaweza kufanya mabadiliko makubwa ya yupi anaye faa kuwa kiongozi na yupi asiye faa.

Tusiendekeze ushabiki wa vyama vya siasa tuangalie nchi imetoka wapi?iko wapi na inakwenda wapi? ,tusijisahau tuwe makini sana ni yupi anafaa kuwa kiongozi wa taifa hili,pia hizi mbwembwe na vituko vya kampeni tuviangalie kwa jicho la tatu sababu hawa wagombea wanafanya hivyo ili kila mmoja aonekane ni bora kuliko mwingine.

Watanzania amka piga kura kwa kiongozi bora na si bora kiongozi taifa letu litajegwa na na wewe mwananchi.

"Mtazamo wangu"

Tuesday, 25 August 2015

Kampeni za kushitukiza marufuku-KOVA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku wagombea urais kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.

Akiongea Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo Suleiman Kova ametolea mfano kitendo cha mgombea urais wa Chadema Mhe. Edward Lowassa cha kufanya ziara ya kushtukiza kwa wananchi na kupanda daladala.

Amesema ziara hiyo ya Mhe. Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji walitembelea Gogo la Mboto, ingeweza kuhatarisha usalama wa wananchi kwa kuwa watu wengi walikusanyika na wengine kuacha kazi zao.

Epuka tabia hizi katika maisha

#Kutarajia Mabadiliko ya Ghafla Kwenye Maisha. 

Mabadiliko yoyote yale kwenye maisha ya kila siku ni mchakato wa taraatibu sana,Hakuna mbadiliko ya ghafla.Kila jambo lina hatua zake muhimu kuelekea kwenye kilele chake cha mabadiliko hakuna jambo ambalo linatokea ghafla na likabadilika ghafla.Mfano Mzuri Tangu Mwanadamu anapozaliwa Mpaka anapofikia hatua ya Utu Uzima.Kila Jambo kwenye maisha yake huenda taratibu na kwa kufwata hatua muhimu.Hatua Moja ya Nyuma humuandaa mwanadamu kwa ajili ya hatua nyingine muhimu ya maisha yake ya mbele. Maisha yetu ya kila siku ni mchakato usiokuwa na mpinzani maana sheria za asili ziliwekwa vivyo hakuna anayeweza kuzipindua maana sheria hizo ndio zinazolinda na kuhakikisha uhai unatunzwa.Mabadiliko yoyote yakifwata mchako huwa yanakuwa na athari mbaya kwa muhusika ambaye mabadiliko hayohutokea.Ni muhimu kuishi kwa kutambua mabadiliko ni mchakato na sio jambo la ghafla. 


#kufikiria kila Mtu atakubaliana na Wewe Kwa Kila Jambo. Mara nyingine kwenye maisha,taaluma,biashara ,maeneo ya kazi huwa tunatarajia kila jambo tunalolifanya,tunalosema na kulifanya ni lazima likubalike na wote.Ni muhimu kutambua kwamba chochote unachofanya kwenye maisha yako wewe ndio unakielewa zaidi kuliko watu wa nje wanaokuzunguka ni muhimu kutambua na ili uweze kuishi maisha ya furaha ujue kwamba si kila jambo unaweza kukubalika na watu wote.Binadamu tumetofautiana namna tunavyofikiria na namna tunavyofanya mambo kadha wa kadha muda mwingine ni ngumu kukubalia katika kila jambo ni lazima utofauti utajitokeza tu maana hatutumia mfumo mmoja wa kufikiria na namna ya kufanya vitu.Unapoona mtu anatofautia na wewe kimtazamo au kwa namna nyingine yeyote ile basi tambua ni wakati muafaka wa kujifunza kwa mtu huyo bila kinyongo,wivu,husuda na kejeli. 


#kutarajia Kila Mtu Atakuheshimu. 

Muda mwingine tumekuwa na misongo ya mawazo isiyokuwa na ulazima kwa sababu ya matarajio finyu na mbaya ambayo muda mwingine tumeyatarajia kutoka kwa wengine.Ni muhimu kutambua si kila mtu ana uwezo wa kuheshimu kuthamini kile unachokifanya kwenye maisha yako ya kila siku.Wapo watu ambao watakukosoa,wapo ambao watakudharau,wapo ambao watakudhalilisha kulingana na sababu wanazozijua wao.Hakikisha haujijengei mawazo kwamba kila unalofanya lazima kila mtu aliheshimu.Tunapoishi hapa ulimwenguni tumetofautiana na kila mtu ana namna yake ya kufanya vitu na namna ya kutafsiri vitu pia mfumo wa malezi tangu tukiwa wadogo umetutofautisha sana mpaka tulipofikia kwa sasa.
Ni muhimu kutojiamini kupita kiasi kwamba kila mtu ana uwezo wa kukuheshimu kwenye kila jambo unalofanya maishani mwako. 


#Kufikiria kwamba Wengine Wanatambua Kile Unachofikiria. 

Hakuna mtu anayeweze kufikiria na kubuni kitu kingine ambacho kipo kwenye akili ya mtu mwingine.Muda mwingine tumekuwa na magomvi yasiyokuwa na ulazima sababu tumekuwa tukifikiri kana kwamba watu wengine wanatambua kile kilichopo ndani mwetu na huwa hawajali kabisa.Iwapo haukuzungumza kwa umakini na utararibu mzuri wa kuwa wezesha wengine kile kilichomo ndani mwako ni ngumu kutambua.Njia rahisi ya kuweza kuwafanya wengine waelewe na kuwa pamoja na wewe kwenye mambo kadha wa kadha ni kuhakikisha unawaeleza kile kilichomo ndani mwako na kipi unafikiria kifanyike.Kila mtu ana mawazo na mfumo wa maisha yake na pia ana namna amvyochakata habari ndani mwake.
Ni muhimu kujenga uweza wa kuwaeleza wengine kile ndani mwako bila wewe ku kilichomo buni kwamba wao watakuwa wanafahamu tu.

Imetoka Gospel Kitaa

Baada ya jana kupanda daladala leo kaendelea na kampeni

Mgombea urais wa UKAWA kwa tiketi ya chama cha chadema mh.Edward Lowasa ameendelea na kampeni zake jijini Dar es salaam ambapo jana alipanda mabasi ya abiria ikiwa ni kutaka kujua matatizo wanayokutana nayo.

Leo ameendelea na kampeni zake ambapo ameenda katika soko la tandale na kujionea hali halisi ya soko hilo.
Tutaendelea kukupasha habari za kisiasa kila wakati endelea kuwa nasi #shangwetz.blogspot.com

Monday, 24 August 2015

Zaidi ya masaa 8 kampenzi za CCM

Chama cha mapinduzi,CCM kimezindua kampeni zake za kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu jana alizindua kampeni jijini Dar es Salaam katika tukio ambalo liliwavuta wanachama na wafuasi na mashabiki wa chama hicho kwa mda zaidi ya masaa manane.

Uzinduzi huo ambao ulikuwa na ulinzi mkali ulikuwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU),ambao walisambazwa katika kona zote za uwanja huo kuimarisha ulinzi. 

Viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali walijitokeza katika uzinduzi huo wa kampeni za chama tawala ambao ulipambwa na wasanii wa Bongo fleva.

Miongoni mwa viongozi hao ni mawaziri wakuu wastaafu, Dk Salim Ahmed Salim na  Jaji Joseph Warioba, rais wastaafu,  Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar na Dk Ali Mohamed Shein. Wengine ni katibu mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula

Baadhi ya viongozi waliopewa nafasi ya kuzungumza na Mkapa alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema kati ya watu wanane waliopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwania urais, timu nzuri ni ile ya mgombea wa CCM, Dk Magufuli na mgombea mwenza, Samia. Alisema Tanzania kuna chama kimoja tu cha ukombozi ambacho ni CCM nakuwataka watanzania kupigia kura zote chama cha ccm.:

Sunday, 23 August 2015

HAWEZI KUKUACHA KAMWE

KATIKA hali zote inatakiwa mkristo uelewe Yesu hawezi kukuacha umpweke kwani yupo ili kuondoa hali zote zilizopotea na kukuhuisha maisha yako kwa upya.

Hayo yalisemwa na Mtumishi wa Mungu Bernie Gillott wa huduma ya Global teen challenge iliyopo nchini Marekani alipokuwa akihubiri katika kanisa la Dar Calvary Temple Tabata Shule.

Alisema wakristo wengi ambao wapo katika wokovu hupitia katika hali tofauti za maisha hususani wapatwapo na majaribu na ambapo hudiliki kusema kuwa Mungu amewaacha na wakati mwingine hawapati wa kuwafariji na kuwatia moyo lakini cha msingi haina haja ya kuona umeachwa elewa Mungu yupo nawe wakati wote kwani yeye alikujua hata kabla ya kuzaliwa kwako(Yeremia 49:11)

Mtumishi wa Mungu Gillott alisema wakati mwingine inashangaza baadhi ya watu kusikia wanasema ee Mungu mbona sasa mimi hunipi ushuhuda? ila tatizo ni kutokuelewa kuwa mtu unapokuwa katika majaribu hapo ndipo njia pekee inayopelekea mtu kutoa ushuhuda baada ya kushinda majaribu.

Unapo kuwa na jaribu na kuona na kukutana na makundi mengi ya kukatisha tamaa na kutengwa elewa Yesu yupo njiani katika hali zote kukupa msaada, Yesu alipo kwenda mji wa Naini alimuonea huruma yule mama mjane aliyefiwa na mtoto wake wa pekee na kusikia kilio chake ambapo alifufua maiti ile na kutoa faraja kwa mama mjane (Luka 7:11-15).

Alipo Yesu elewa huondoa hali ya upweke na huhuisha tena maisha hali zote zilizopotea, kama alivyo sikia kilio cha mama mjane na huo ni udhibitisho wa upendo? wake kwetu kwa kujitoa pale calvary alipoleta ukombozi kwa mwanadamu, kwani yeye ni Mungu wa marejesho katika hali zote za maisha zilizopotea na siku zote hukutana na watu walioko dhambini na walio potea Zaburi 68:1-3,Yeremia 49:11 na zaburi 146:9

Monday, 10 August 2015

PICHA 7 ZA GUMZO MAANDAMANO UKAWA

Hizi ni picha zikionyesha idadi kubwa ya watu katika maandamano yaliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam ya mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh. Edward Lowasa alipokuwa anaenda kuchukua fomu ya kugombea kuwakilisha umoja wa katiba UKAWA.

Maandamano makubwa yaliyofanyika na kuwa na wananchi wengi inasemekana haijawahi kutokea nchi isopokuwa ni yale yaliyokusanya wananchi kama hao katika msiba wa Baba wa Taifa JK . Nyerere