Pages

Sunday, 23 August 2015

HAWEZI KUKUACHA KAMWE

KATIKA hali zote inatakiwa mkristo uelewe Yesu hawezi kukuacha umpweke kwani yupo ili kuondoa hali zote zilizopotea na kukuhuisha maisha yako kwa upya.

Hayo yalisemwa na Mtumishi wa Mungu Bernie Gillott wa huduma ya Global teen challenge iliyopo nchini Marekani alipokuwa akihubiri katika kanisa la Dar Calvary Temple Tabata Shule.

Alisema wakristo wengi ambao wapo katika wokovu hupitia katika hali tofauti za maisha hususani wapatwapo na majaribu na ambapo hudiliki kusema kuwa Mungu amewaacha na wakati mwingine hawapati wa kuwafariji na kuwatia moyo lakini cha msingi haina haja ya kuona umeachwa elewa Mungu yupo nawe wakati wote kwani yeye alikujua hata kabla ya kuzaliwa kwako(Yeremia 49:11)

Mtumishi wa Mungu Gillott alisema wakati mwingine inashangaza baadhi ya watu kusikia wanasema ee Mungu mbona sasa mimi hunipi ushuhuda? ila tatizo ni kutokuelewa kuwa mtu unapokuwa katika majaribu hapo ndipo njia pekee inayopelekea mtu kutoa ushuhuda baada ya kushinda majaribu.

Unapo kuwa na jaribu na kuona na kukutana na makundi mengi ya kukatisha tamaa na kutengwa elewa Yesu yupo njiani katika hali zote kukupa msaada, Yesu alipo kwenda mji wa Naini alimuonea huruma yule mama mjane aliyefiwa na mtoto wake wa pekee na kusikia kilio chake ambapo alifufua maiti ile na kutoa faraja kwa mama mjane (Luka 7:11-15).

Alipo Yesu elewa huondoa hali ya upweke na huhuisha tena maisha hali zote zilizopotea, kama alivyo sikia kilio cha mama mjane na huo ni udhibitisho wa upendo? wake kwetu kwa kujitoa pale calvary alipoleta ukombozi kwa mwanadamu, kwani yeye ni Mungu wa marejesho katika hali zote za maisha zilizopotea na siku zote hukutana na watu walioko dhambini na walio potea Zaburi 68:1-3,Yeremia 49:11 na zaburi 146:9

No comments:

Post a Comment