Pages

Tuesday, 25 August 2015

Epuka tabia hizi katika maisha

#Kutarajia Mabadiliko ya Ghafla Kwenye Maisha. 

Mabadiliko yoyote yale kwenye maisha ya kila siku ni mchakato wa taraatibu sana,Hakuna mbadiliko ya ghafla.Kila jambo lina hatua zake muhimu kuelekea kwenye kilele chake cha mabadiliko hakuna jambo ambalo linatokea ghafla na likabadilika ghafla.Mfano Mzuri Tangu Mwanadamu anapozaliwa Mpaka anapofikia hatua ya Utu Uzima.Kila Jambo kwenye maisha yake huenda taratibu na kwa kufwata hatua muhimu.Hatua Moja ya Nyuma humuandaa mwanadamu kwa ajili ya hatua nyingine muhimu ya maisha yake ya mbele. Maisha yetu ya kila siku ni mchakato usiokuwa na mpinzani maana sheria za asili ziliwekwa vivyo hakuna anayeweza kuzipindua maana sheria hizo ndio zinazolinda na kuhakikisha uhai unatunzwa.Mabadiliko yoyote yakifwata mchako huwa yanakuwa na athari mbaya kwa muhusika ambaye mabadiliko hayohutokea.Ni muhimu kuishi kwa kutambua mabadiliko ni mchakato na sio jambo la ghafla. 


#kufikiria kila Mtu atakubaliana na Wewe Kwa Kila Jambo. Mara nyingine kwenye maisha,taaluma,biashara ,maeneo ya kazi huwa tunatarajia kila jambo tunalolifanya,tunalosema na kulifanya ni lazima likubalike na wote.Ni muhimu kutambua kwamba chochote unachofanya kwenye maisha yako wewe ndio unakielewa zaidi kuliko watu wa nje wanaokuzunguka ni muhimu kutambua na ili uweze kuishi maisha ya furaha ujue kwamba si kila jambo unaweza kukubalika na watu wote.Binadamu tumetofautiana namna tunavyofikiria na namna tunavyofanya mambo kadha wa kadha muda mwingine ni ngumu kukubalia katika kila jambo ni lazima utofauti utajitokeza tu maana hatutumia mfumo mmoja wa kufikiria na namna ya kufanya vitu.Unapoona mtu anatofautia na wewe kimtazamo au kwa namna nyingine yeyote ile basi tambua ni wakati muafaka wa kujifunza kwa mtu huyo bila kinyongo,wivu,husuda na kejeli. 


#kutarajia Kila Mtu Atakuheshimu. 

Muda mwingine tumekuwa na misongo ya mawazo isiyokuwa na ulazima kwa sababu ya matarajio finyu na mbaya ambayo muda mwingine tumeyatarajia kutoka kwa wengine.Ni muhimu kutambua si kila mtu ana uwezo wa kuheshimu kuthamini kile unachokifanya kwenye maisha yako ya kila siku.Wapo watu ambao watakukosoa,wapo ambao watakudharau,wapo ambao watakudhalilisha kulingana na sababu wanazozijua wao.Hakikisha haujijengei mawazo kwamba kila unalofanya lazima kila mtu aliheshimu.Tunapoishi hapa ulimwenguni tumetofautiana na kila mtu ana namna yake ya kufanya vitu na namna ya kutafsiri vitu pia mfumo wa malezi tangu tukiwa wadogo umetutofautisha sana mpaka tulipofikia kwa sasa.
Ni muhimu kutojiamini kupita kiasi kwamba kila mtu ana uwezo wa kukuheshimu kwenye kila jambo unalofanya maishani mwako. 


#Kufikiria kwamba Wengine Wanatambua Kile Unachofikiria. 

Hakuna mtu anayeweze kufikiria na kubuni kitu kingine ambacho kipo kwenye akili ya mtu mwingine.Muda mwingine tumekuwa na magomvi yasiyokuwa na ulazima sababu tumekuwa tukifikiri kana kwamba watu wengine wanatambua kile kilichopo ndani mwetu na huwa hawajali kabisa.Iwapo haukuzungumza kwa umakini na utararibu mzuri wa kuwa wezesha wengine kile kilichomo ndani mwako ni ngumu kutambua.Njia rahisi ya kuweza kuwafanya wengine waelewe na kuwa pamoja na wewe kwenye mambo kadha wa kadha ni kuhakikisha unawaeleza kile kilichomo ndani mwako na kipi unafikiria kifanyike.Kila mtu ana mawazo na mfumo wa maisha yake na pia ana namna amvyochakata habari ndani mwake.
Ni muhimu kujenga uweza wa kuwaeleza wengine kile ndani mwako bila wewe ku kilichomo buni kwamba wao watakuwa wanafahamu tu.

Imetoka Gospel Kitaa

No comments:

Post a Comment