Katika hali isiyo ya kawaida katika mkutano wa UKAWA kupitia mgombea wake wa uraisi kupitia Chadema mh. Edward Lowassa ametoa ahadi kwa watanzania kuwa miongoni mwa vitu atakavyo vitolea maamuzi iwapo wakimpa nafasi ya kuiongoza nchi, atawatoa gerezani baadhi ya wafungwa na wawe huru.
Mh. Lowassa aliongea hayo katika ufunguzi wa kampeni za ukawa jijini Dar es salaam viwanja vya jangwani.
Lowassa baada ya kutaja ilani za ukawa alimalizia kwa kusema atahakikisha anamtoa gerezani Babu Seya pamoja na mashekhe ambao wamefugwa gerezani.
Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na mtoto wake walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto mwaka 2010.
Katika kesi yao Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana nahatia walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kuwa mwanamuziki huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa baada ya kukata rufaa kwa ombi lake la mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment