Uzinduzi huo ambao ulikuwa na ulinzi mkali ulikuwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU),ambao walisambazwa katika kona zote za uwanja huo kuimarisha ulinzi.
Viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali walijitokeza katika uzinduzi huo wa kampeni za chama tawala ambao ulipambwa na wasanii wa Bongo fleva.
Miongoni mwa viongozi hao ni mawaziri wakuu wastaafu, Dk Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba, rais wastaafu, Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar na Dk Ali Mohamed Shein. Wengine ni katibu mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula
Baadhi ya viongozi waliopewa nafasi ya kuzungumza na Mkapa alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema kati ya watu wanane waliopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwania urais, timu nzuri ni ile ya mgombea wa CCM, Dk Magufuli na mgombea mwenza, Samia. Alisema Tanzania kuna chama kimoja tu cha ukombozi ambacho ni CCM nakuwataka watanzania kupigia kura zote chama cha ccm.:
No comments:
Post a Comment