Pages

Friday 8 April 2016

WHATSAPP KULINDA MAWASILIANO YA WATEJA WAKE

Huduma ya ujumbe Whatsapp imetangaza kuwa itayalinda mawasiliano ya wateja wake kuanzia hapo siku ya Jumanne wiki hii.
Huku ulinzi ukiwekwa mwanzo na mwisho wa ujumbe ujumbe ukaharibiwa wakati unapotoka katika simu ya anayeutuma na unaweza kusomwa pekee na anayeupokea.

Hatua hiyo utaufanya ujumbe huo kutosomeka iwapo mhalifu ama hata maafisa wa polisi wanajaribu kuingilia simu bila ya idhini kutoka kwa mhusika mwenye simu.

WhatsApp ambayo ina wateja zaidi ya bilioni moja duniani imesema kuwa uhamisho wa faili pamoja na sauti pia zitalindwa.

Huduma hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Facebook imesema kuwa ulinzi wa mawasiliano ya faragha ni miongoni mwa malengo yake.

Ulinzi huo uliathiriwa wakati shirika la Marekani la FBI lilipotaka kampuni ya Apple kuisadia kuchukua data katika simu moja ya iPhone iliotumiwa na muuaji Syed Farook.

Whatsapp ilisema, "Wazo hilo ni rahisi, unapotuma ujumbe mtu pekee anayeweza kuusoma ni mtu ama kundi la mawasiliano ambalo umelitumia ujumbe huo."
"Hakuna mtu anayeweza kuusoma ujumbe huo hata kama ni wahalifu wa mitandaoni au hata serikali, hata sisi hatuwezi kuusoma," waliongezea.

Watumiaji wapya wa huduma hiyo waliarifiwa kuhusu mabadiliko hayo wakati wanapotuma ujumbe siku ya Jumanne.

MAGAZETI YA LEO APRIL 12, 2016