Pages

Wednesday 9 September 2015

Jinsi ya Kukabiliana na Msongo wa Mawazo/Stress

Msongo wa Mawazo/Stress ni tatizo ambalo limeendelea kuwa tatizo sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo,Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili.
Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi,lakini jambo la baraka ni kuwa msongo wa mawazi unaepukika,hivyo
Ungana nami ili kujua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo.

Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili.

Kuzingatia hilo kuna mambo kadha wa kadha yanayomkabili kila mwanadamu
#  Kutojiamini
#  Kuogopa mabadiliko
#  Kukosa mpango wa maisha
#  Kupuuza mahitaji muhimu ya binadamu ya:-  Mwil,  Roho, Akili
#  Kuishi kwa kukata tama•Kuumwa kichwa, Kukosa nguvu za mwili (me+ke),  Matatizo makubwa ya familia, Kukosa upendo,Hasira za mara kwa mara, Waathirika wa msongo na kusambaratika


Kila lika inakubwa na tatizo hili la Msongo wa Mawazo lakini nitajaribu kufafanua watu tofauti ambao hukubwa sana na tatizo hili

Wazazi – sababu kubwa ni uchumi wa familia: Watoto wanaouwezo wa kukuhoji kwa nini wewe ni masikini, kushindwa kupeleka watoto shule, kushidwa kutatua matatizo hata madogo madogo ya Familia hapo lazima upate Msongo wa Mawazo.


Waajiri/Waajiriwa – Watu hawa hupatwa na tatizo hili na huwapelekea kuhamisha mambo ya kazini
wanapeleka nyumbani na ya nyumbani wanayapeleka kazini. Mfano mtu amegombana na wafanyakazi wenzake kwa makosa yake mwenyewe akarudi nyumbani na kuendelea na hali ile na kusababisha matatizo nyumbani kwake.

Vijana na wanafunzi – Vijana wengi hukubwa na tatizo hili hasa katika maswala ya kiuchumi na kwa wanafunzi wengi kuingia katika Mapenzi wakiwa bado wapo shule huwasababishia msongo wa mawazo kwani tayari anakua kajipa majukum mengine. Mfano jana amegombana na mpenzi wake leo akienda shule hawezi kusoma vizuri atakua mtu mwenye mawazo kutokana na kilichomkuta siku iliyopita.

Wanandoa – Wanandoa wengi  wana msongo na kukosa faraja. Wanaamini nje kuna faraja zaidi (nyumba ndogo)
Wakristo wanaweza kusoma vitabu hivi ili kupata maelezo (luka 24),  (matendo 11:28-30),  (yohana 18:14-27)

Mizigo inayochosha
# Watu wengi hupata Msongo wa mawazo kutokana na wao kutaka

# kujitwika mizingo wasiyo weza kuibeba nitataja baadhi Kushindana na jirani
# Kufanya mambo nje ya uwezo wako
Kupata bp, tumbo, kichwa, bila sababu
# Kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao huwezi kuwalea


Msongo wa mawazo hujitambulisha sana kwa mwili, akili na roho

Akili – ikisikia juu ya jambo gumu inashindwa kulipokea.  Inapeleka kwa tumbo, tumbo linashindwa linaamua kutoa unaharisha ndipo mtu hupata vidonda vya tumbo na tumbo kupata maumivu makali.

JINSI YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO

      Jifunze Kukubali Changamoto, Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.

      Jifunze kusema "hapana" hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.

        Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, Kunawakati huwa tunakua na kampani ya watu ambao kabisa unajua hawa wananisababishia msongo wa mawazo Mfano:- Upo katika mahusiano na mtu ambaye wewe unampenda lakini haonyeshi kujali upendo wako utajitahidi kupiga simu kutuma sms umweke karibu lakini yeye hajali, si busara ukaendelea kuumiza kichwa kwajili yake ni bora uachane nae mapema sana. Pia hata marafi wapo maadhi ya marafiki wanaweza wakakusababishia msongo wa mawazo kutokana na wanayokufanyia kwa mfano rafiki anayekupenda wakati wa raha tu na anakukimbia ukiwa na shida huyo si mwema kwako atakufanya uwe na Msongo wa mawazo. Tembelea watu wanaokufanya ufurahi na jifunze kucheka na kufurahi. Epuka kakaa na watu ambao kwako ni kikwazo.

       Panga kazi zako kwa ratiba usivuruge ratiba kwa vitu visivyo vya lazima ili kumfurahisha mtu mwingine. Mfano:- Umeapanga ratiba yako ya siku nzima anakuja rafiki ako akakuomba umsindikize sehemu ambayo haina umuhimu wala ulazima ukaenda ukapoteza mda mwingi huko, ukirudi tayari unakua umejipa Msongo kwani ratiba yako itakua imevurugika na utajilazimisha hata kuchelewa kulala ili tu umalize uliyo panga. Hiyo inaweza kukupa msongo kwani utakua ukifanya vitu kwa manung'uniko. katika ratiba yako tenganisha ratiba hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa mawazo.

      Epuka Hasira za haraka, kuna mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka kukaa nao karibu ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi

      Fanya kazi yako ya halali kwa juhudi na maarifa

      Uwe na malengo ya maisha.  Fanya jambo moja kwa wakati wake. Mfano jiulize unataka kufanya nini kwa wakati gani na ili uwe nani?

      Wakati unapokula usiwe unaonngea au kukumbuka shida zako.  Pia kula polepole na kwa raha zako.  Ikiwezekana wakati wa kula zima simu. kwasababu tunajua hatuwezi kuishi bila kula tujaribu kuheshimu mda wa kula kwani kunawakati hata simu zetu tunaweza kupokea kitu kikatufanya tuvuruge hata ratiba ya kula na kupoteza hamu na kusababisha Msongo wa mawazo.

       Fanya mazoezi kila siku, mara tano angalau kwa juma tofautisha kazi na mazoezi.

       Sikiliza muziki wa injili, bongo flava, lugha yenu ya asili, muziki ni dawa, nchi za afrika ziliponya kwa muzik (Afrika kusini na Kongo)

         Tafuta sababu zinazokuletea msongo wa mawazo, zitambue na kuzifahamu ili uziepuke.

        Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni, Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.

        Usiweke Malengo ambayo Hayafikiki, Kila mtu ana uwezo na vipawa vyake tofauti na mtu mwingine, unapoweka malengo yako hakikisha unazingatia uwezo, vipawa na muda ulionao ili kuweza kuyafanikisha. Usiweke malengo sababu watu wengine wameweka hayo,au ukaweka muda kiasi fulani sababu watu wote wameweka hivyo, daima zingatia uwezo wako ili malengo yako yaweze kufanikiwa na kuepuka kupata 'stress'.
   
      Fanya Maamuzi Pale Unapopaswa
Kutokufanya maamuzi katika muda sahihi hyleta wasiwasi hofu na msongo wa mawazo. Uwe na ujasiri wa kuamua mara baada ya kutafakari pande zote kwa makini na kuona faida na hasara za kila upande. Usihofu sana juu ya kuweza kufanya makosa hadi ukaishia kupata msongo wa mawazo, mara nyingine watu hujifunza kutokana na makosa.

    Kuwa na Mipango,Hili nimeshaliongelea sana, angalia hapa Kutokuwa na mipango ni sababu moja kubwa sana inayoweza kukuletea msongo wa mawazo.


    Jali Mwili Wako,  mara nyingi tunakuwa na shughuli nyingi kiasi cha kuusahau mwili na kuuchukulia tu kwa juu juu. Ni muhimu sana mwili wako uwe katika hali nzuri na afya bora ili uweze kufanya kazi zako vizuri na kwa wepesi. Hakikisha unakula chakula chenye virutubisho bora na pia unakunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku.

@chanzo mtandao

No comments:

Post a Comment