Pages

Friday 25 September 2015

UKAWA WAKOSOA UTAFITI WA TWAWEZA

Umoja Wa Vyama vinavyounda UKAWA wasema utafiti wa Twaweza hauna ukweli, akizungumza kwa niaba ya UKAWA,Mwenyekiti Wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia alisema kuwa taarifa ya taasisi hiyo imeidhalilisha TWAWEZA wenyewe na CCM kwa ujumla.
Aidha utafiti wa TWAWEZA umekuwa ni utafiti wakiubaguzi kubagua wagombea urais Wa vyama vingine mbali na CCM na CHADEMA"

"Katika taarifa ya TWAWEZA haijaweza kuhakiki taarifa yake kitakwimu,CCM imekubaliana na idadi ya watu walioshiriki kwenye utafiti kwa kigezo cha idadi ya watu 1848"
"CCM hiyo hiyo ilikataa kukubali maoni ya wananchi zaidi ya laki tatu kwenye rasimu ya katiba ya Warioba,lakini leo wamekubali watu 1848" aliongeza Mbatia.

"TWAWEZA wanajua vyama vya CUF,NCCR-MAGEUZI,na NLD hawajatoa wagombea wao Wa urais isipokuwa CHADEMA ila wameweka swali hilo,kwakuwa TWAWEZA ni taasis inayothamini midahalo tunawaalika kwenye midahalo ya kutetea taarifa ya utafiti wao".
"Utafiti Wa ndani Wa UKAWA uliofanywa na watafiti guru kutoka nje ya nchi ulionyesha Edward Lowassa atapata kura 74%".alisema Mbatia.
Naye Prof.Baregu alisema kuwa sampuli ya data za utafiti Wa TWAWEZA imechafuliwa kwa makusudi ili kupotosha umma.
"Mtafiti kutoka Oxford University niliongea naye aliona kuwa UKAWA inaweza kushinda ila siyo kwa gap kubwa"alisema Baregu





No comments:

Post a Comment