Pages

Thursday 31 March 2016

SERIKALI YA JAPANI YAIPIGA TAFU TANZANIA KWA ZAIDI YA BIL. 116.

Tanzania imepokea msaada toka serikali ya Japan msaada wa Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili unahusu masuala ya kiufundi yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500

Monday 28 March 2016

TFF NAYO YADHIBITISHA TIMU YA CHAD KUJIENGUA MICHUANO YA AFCON 2017

Shirikisho la Soka nchini TFF
limethibitisha taarifa yetu ya awali
kwamba timu ya Taifa ya Chad ' Les Sao ' imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika ( AFCON ) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon .

Tovuti ya TFF inasema kwamba taarifa ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika ( CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania , Nigeria na Misri.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza mchezo wa awali jijini N' Djamena katika ya wiki.

Katika mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Idriss Mahamat Ouya , Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1 - 0 , bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo .

Kufuatia kujitoa kwa Chad, matokeo ya michezo yote iliyoihusisha timu hiyo yanafutwa , na msimamo wa kundi G kwa sasa unaongozwa na Misri yenye pointi 4 , Nigeria pointi 2 na Tanzania pointi 1 .

Sunday 27 March 2016

TIMU YA CHAD YAJIENGUA AFCON 2017

Timu ya Taifa ya Chad 'Les Sao' imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.

Taarifa ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoa katika mashindano hayo ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri.

Chad ilitarajiwa kucheza Leo Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza mchezo wa awali jijini N'Djamena katika ya wiki.

Katika mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Taifa Taifa Stars ingecheza mchezo wake wa pili wa marudiano na Chad leo Jumatatu ya March 28 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam , baada ya mchezo wa kwanza kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MARCH 28,2016

Rais John Pombe Magufuli:watanzania Tusibaguane.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuendeleza umoja na mshikamano na kutobaguana.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front Jijini Dar es salaam, ambako amesali ibada ya Pasaka pamoja na waumini wa kanisa hilo.

Amesema Mwenyezi Mungu alimtoa mwanae wa pekee Yesu Kristo kuja kuikomboa dunia bila kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu tunapaswa kutobaguana, iwe kwa dini zetu, makabila yetu, mitazamo ya kisiasa na hata rangi zetu.

Hata hivyo alisisitiza watu kufanya kazi kwa bidii,
"Tukifanya kazi hatuhitaji hata misaada kutoka nje, nchi hii ina neema nyingi. Kwa kweli tukifanya kazi kwa bidii nchi yetu inapaswa kuwa inatoa misaada kwa nchi nyingine na sio kuomba misaada kutoka nchi nyingine" Amesisitiza Dkt. Magufuli.

Rais Magufuli ambaye amesali kwenye kanisa hilo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ikiwa ni mara yake ya nne kusali katika kanisa hilo hata kabla ya kuwa Rais, amewaomba watanzania kuendelea kuliombea Taifa lao na pia kumuombea yeye ili afanikiwe kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza nchi.
Pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli waliohudhuria ibada hiyo,

Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa amempongeza Rais Magufuli kwa tabia yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi viongozi wengine kupenda ibada.

Askofu Malasusa ameuelezea ufufuo wa Yesu Kristo kuwa jambo la kuleta matumaini, na hivyo amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa, huku akisema Kanisa linaona matumaini