Pages

Thursday 10 March 2016

FAIDA ZA KULA TUNDA LA TIKITI MAJI

Tikiti maji ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi hapa nchini kwetu;tunda hili mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.

Vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu ikiwa asilimia 92 ya tikiti maji huwa ni maji na asilimia 8 zilizobakia zina faida kubwa sana kiafya jambo halifahamiki na wengi wetu.

Ebu kwa uchache hizi ni baadhi ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:

Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho pia kuondosha sumu mwilini.

Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.

Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani;ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.

Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.

Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.

Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine; Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.

No comments:

Post a Comment