Pages

Wednesday 2 March 2016

UMUHIMU WA MACHUNGWA KWA AFYA

Machungwa ni miongoni mwa matunda maarufu yanayolimwa sehemu mbalimbali nchini na duniani na matunda hayo ni jamii ya matunda aina ya citrus na  inajumuisha machungwa na machenza n.k

Watu wengi wamekuwa hawana utamaduni wa kula matunda wakati mwingine sio kwa kukosa uwezo wa kuyanunua ila ni kupuzia na wengine kutokujua umhimu wake katika afya ya binadamu.

Ukiwa na utamaduni wa kula matunda hakika utakuwa mtu wa tofauti hususani machungwa kwa kuwa kuna Virutubisho ndani ya machungwa.

Kazi ya machungwa katika mwili wa binadamu ni chanzo kikubwa  cha Vitamini C katika mlo, Chungwa lenye ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na miligramu 75 kwa mwanamke.

Vitamini C iliyomo kwenye chungwa huimalisha uzalishaji wa Seli hai nyeupe zinazoimalisha kinga mwilini na unapokuwa na kinga imara huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.

Machungwa yaweza kuliwa au kutengenezea juisi, kwani juisi yake huwa na virutubisho vyote vya machungwa isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi mtu napokula chungwa zima.

Inashauriwa kula chungwa moja au mawili kwa siku, kwani hii hutosheleza mahitaji ya Vitamin mwilini.

Aidha machungwa huimarisha afya ya fizi na mdomo;Vitamini C husaidia kujenga protini za kolajeni za fizi za mdomoni, hii huimarisha afya ya fizi. Ukosefu wa Vitamini C mara nyingi huambatana na fizi kuvuja damu kutokana na kukosa protini za kolajeni za kutosha.

#Afyakwanza.

No comments:

Post a Comment