Pages

Wednesday 26 August 2015

Kura yako moja ithamini chagua kiongozi makini

Mtanzania ni siku chache zimebaki kufikia october  tutapiga kura kuchagua viongozi watakao shika madaraka ya kuongoza  taifa hili la Tanzania lenye kusifiwa duniani kwa kudumisha amani na utulivu.

Lakini pamoja na hayo leo nimekuja na swali dogo la msingi sana"JE UNATAKA KUWA NA TANZANIA YA NAMNA GANI 2015-2020?"bila shaka jiulize swali hilo kisha jijibu mwenyewe,tunapoelekea katika uchaguzi mkuu ni wakati tunapaswa kuwa makini sana kwenye kampeni za wanasiasa  wanavyo nadi ilani za vyama vyao kwetu wananchi inapaswa tufuatilie kwa umakini kwa lengo la kujue ni nini lilichomo humo.


Nasema hivyo kwasababu kampeni za mwaka huu zimekuwa za ushindani sana na wananchi wako mstali wa mbele katika ufuatiliaji na baadhi yao wamekuwa na mitazamo tofauti inayo ashiria wanajua yupi kiongozi bora hata ukiachana  na ilani za vyama husika.

Hivyo mtanzania mwenzangu hatima ya taifa letu iko mikononi mwako,namanisha sasa hivi ni mda wa kutafakari kwa umakini na kuchuja sera za wagombea ili kujua nani ni nani atafaa kupigiwa kura October.

Kura yako moja ni bidhaa hadimu tunza kadi yako na mwisho wa siku inatakiwa umpigie kura mgombea ambaye utakuwa umeridhishwa naye na kuona anafaa kusimamia rasilimali za nchi hii zikawanufaisha watanzania wote.

Mwananchi amka kura yako moja inauthamani mkubwa sana kwani ndio inaweza kufanya mabadiliko makubwa ya yupi anaye faa kuwa kiongozi na yupi asiye faa.

Tusiendekeze ushabiki wa vyama vya siasa tuangalie nchi imetoka wapi?iko wapi na inakwenda wapi? ,tusijisahau tuwe makini sana ni yupi anafaa kuwa kiongozi wa taifa hili,pia hizi mbwembwe na vituko vya kampeni tuviangalie kwa jicho la tatu sababu hawa wagombea wanafanya hivyo ili kila mmoja aonekane ni bora kuliko mwingine.

Watanzania amka piga kura kwa kiongozi bora na si bora kiongozi taifa letu litajegwa na na wewe mwananchi.

"Mtazamo wangu"

No comments:

Post a Comment