Pages

Thursday 26 February 2015

UTAFITI:Je vipofu wanaona nn giza au mwanga?


Mlemavu wa macho



Mwandishi wa BBC Damon Rose alipofuka alipokuwa mtoto lakini anasema kuwa sio kwamba mtu aliyepofuka anaona giza.

Je, yeye anaona nini haswa?

Watu hudhani kwamba watu waliopofuka huona weusi tititi,lakini kulingana na uzoefu wa mwandishi huyu hilo si kweli.
Anasema kwamba kila anapoulizwa ni nini haswa anachokikosa kwa kuwa yeye ni kipofu husema ni giza.
Huo ndio mwanga waonao vipofu




Anasema kuwa yeye ni mmoja ya watu ambao hawaoni kabisa Alipofuka miaka 31 iliopita baada ya kufanyiwa upasuaji ambao haukufaulu.Anasema Rangi wanazoona watu walio pofuka Watu hudhania kwamba mwangaza na unapoondolewa basi mtu husalia katika giza.

''Unapoingia katika matandiko huwezi kuona kitu kabisa.Unapofunga macho kila kitu kinabadilika na kuwa giza''.

''Kwa hivyo upofu ni sawa na giza?
Inaingia maanani lakini si kweli''.

''Ijapokuwa uhusiano wangu wa akili na macho umekatika duniani haijawa giza kwangu.
''.Kwa hivyo unapopofuka ni nini haswa unachoona? aliulizwa
mwandishi huyu. ,''jibu ni mwangaza,mwangaza mwingi sana ,rangi za
kung'ara,rangi nyingi zinazobadilika kila mara na mwangaza mbaya ulio na bughudha''.







Tanzania na Zambia kufufua Reli ya TAZARA

Rais wa Jamhuri ya  muungano wa Tanzania,  Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni nchini Zambia mala baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Edger Lungu (mwenye suti ya kijivu mbele ya Rais Kikwete) 


Nchi ya Tanzania na Zambia zimekubaliana kushirikiana kuimarisha sekta ya miundo mbinu hususani ya kufufua Reli inayounganisha nchi hizi mbili (TAZARA) ili kukuza biashara na uwekezaji.
Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete nchini Zambia.
Akizungumza wakati wa mkutano rasmi kati yake na mwenyeji wake, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais Kikwete alisema kuwa umefika wakati sasa  wa kuifufua Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia.
Mhe. Rais Kikwete alifafanua kuwa umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.
“Upo umuhimu mkubwa wa kuifufua Reli ya TAZARA ili ifanye kazi kama awali kwani ni alama na kiungo muhimu cha ushirikiano wetu sisi Tanzania na Zambia”, alisema Rais Kikwete.
Aidha, aliongeza kuwa Tanzania na Zambia zimekubaliana kuwekeza zaidi katika reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji. 
Alifafanua kwamba hapo awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2 za bidhaa kwa mwaka, wakati sasa reli hiyo inasafirisha  tani laki 2 kwa safari inayotumia hadi siku 12 kutoka Dar es Salaam hadi New Kapiri Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.
“TAZARA inapita katika kipindi kigumu sasa, hivyo tumezungumza namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo uendeshaji na ukarabati ili irejee katika hali yake ya awali”, alisisitiza Rais Kikwete.

Katika  hatua nyingine Mhe. Rais Kikwete alimpongeza Rais Lungu kwa kuchaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa Zambia na pia alitoa salamu za pole kwa Rais huyo na Wazambia wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati Michael Satta.
Kwa upande wake, Rais Lungu alisema kuwa Tanzania na Zambia zinajivunia mafanikio ya ushirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambayo yamejikita katika sekta za Kilimo, Usafirishaji, Nishati na Mawasiliano.
Pia, alisema kwamba nchi yake ipo tayari kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo ambao unaanzia ngazi ya serikali, kanda, Bara  na Kimataifa na kusisitiza umuhimu wa kuitumia Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1992 kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa na nchi hizi mbili. Aidha, alikubaliana na hoja ya kuifufua reli ya TAZARA kwa manufaa ya nchi hizi mbili.
Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini humo kwa mwaliko wa Rais Lungu alifuatana na Mama Salma Kikwete, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini na Mamlaka mbalimbali.

CHID BENZ AHUKUMIWA JELA MIAKA 2 AU KULIPA FAINI YA LAKI 9



Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Tuesday 24 February 2015

Utafiti Simu ya Android

Utafiti umebaini kuwa betri za simu za android zinaweza kutumika kufuatilia watumizi ya Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android kwani zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.
Uchnguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno kutumia kifaa cha GPS yake.
Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake, huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia.
Aidha mbali. na Simu za kisasa ''Smartphone'' hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani inachangamoto tele za kung'amua masafa.
Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubainishwa na ''alogarithm'' muundo msingi wa simu yenyewe.
Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu.
''Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ''
Jopo hilo linajumuishwa Yan Michalevsky, Dan Boneh na Aaron Schulman kutoka idara ya sayansi ya tarakilishi katika chuo kikuu cha
Standford pamoja na Gabi Nakibly kutoka kwa kampuni ya Rafael waliandika katika utafiti wao.
Utafiti umebaini kuwa betri za simu za android zinaweza kutumika kufuatilia watumizi ''Tunaruhusa ya kuunganisha mtandao na upatikanaji wa nguvu yao.''
''Hizi ni ruhusa za kawaida kwa mfumo huo na inawezekano wa kutoleta hutuma kwa upande wa
mwathiriwa.
Kuna mifumo 179 ambazo zinapatikana kwenye Anaroid ,timu hiyo iliongezea. Shughuli kama kuskiza muziki au kutumia
mtandao wa kijamii inamaliza betri ya simu lakin hii inaweza kupunguzwa kutokana na ''kujifunza kwa mashine''ripoti inasema.Jaribio hilo lilifanyiwa kwa simu ambazo zinatumia mtandao wa 3G lakini haikuweza kupima nguvu kwa kuwa twakimu inalindwa na kifaa hicho.






Saturday 14 February 2015

Ufaulu kidato cha nne uko Juu kwa asilimia 10 kwa mwaka 2014

Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa
ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235,227 sawa na 58.25 walifualu.

Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na
mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25 walifualu.

Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.
Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na
asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.
Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa
wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991
sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.
Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia
30.24.

Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.

Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.

Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni:

Kaizirege mkoa wa Kagera
Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
Marian Boys mkoa wa Pwani
St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
Abbey mkoa wa Mtwara
Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
Marian Girls mkoa wa Pwani
Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

Shule 10 za mwisho ni

Manolo mkoa wa Tanga
Chokocho mkoa wa Pemba
Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam
Mashindei mkoa wa Tanga
Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
Vudee mkoa wa Kilimanjaro
Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro
Magoma mkoa wa Tanga.

MATOKEO KIDATO CHA NNE UFAULU WAPANDA ASILIMIA 10

Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa
ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235,227 sawa na 58.25 walifualu
Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa
ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25 walifualu.
Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61
wakati wavulana ni 106,960.
Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni
167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya
mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.

Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa
wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka
2013.
Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991
sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.

Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811
sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.

Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22ikilinganishwa na mwaka 2013.
Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.

Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.

Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni
Kaizirege mkoa wa Kagera
Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
Marian Boys mkoa wa Pwani
St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
Abbey mkoa wa Mtwara
Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
Marian Girls mkoa wa Pwani
Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

Shule 10 za mwisho ni
Manolo mkoa wa Tanga
Chokocho mkoa wa Pemba
Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam
Mashindei mkoa wa Tanga
Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
Vudee mkoa wa Kilimanjaro
Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro
Magoma mkoa wa Tanga.

Dkt Msonde pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni:
Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani
Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam
Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani
Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya
Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel
Memorial Kilimanjaro
Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani
Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa
Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
Mahmoud Bakali kutoka Feza Boys