Pages

Monday 7 September 2015

J.P.MAGUFULI-Watumishi Wazembe kukiona cha Moto.

Mkutano Mkubwa wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa chama cha Mapinduzi CCM mh. John P. Magufuli umeweka kihistoria kwa kuhudhuliwa na idadi kubwa ya watu katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro.

Mgombea huyo wa ccm katika vipaumbele ameahidi akichaguliwa atahakikisha anaondoa nyumba za nyasi/tembe na kutoa Elimu ya kuanzia darasa la kwanza hadi Kidato cha Nne bure

Magufuli alisema mikopo kwa Elimu ya Juu itatolewa kwa haraka bila kuchelewa, watumishi wazembe watawajibishwa, kwani yeye ni mtu wa Kazi tu hatawavumilia viongozi wazembe.

Aliendelea kuahidi akichaguliwa kuwa Rais, wanaomiliki maeneo/viwanja bila kuyaendeleza wawe tayari kuyarejesha

Aidha katika hatua nyingine Rais Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema kuwa Magufuli akichaguliwa ataweza kulala bila wasiwasi kwakuwa anajua ni mtendaji pia ni Mkali, baada ya watanzania kuwa na Rais mpole kama yeye, sasa wanahitaji Rais wa aina ya Magufuli

Kikwete amesisitiza kuwa Lowassa alishiriki katika kupiga kura vikao vya Uteuzi wa mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi CCM.

No comments:

Post a Comment