Pages

Monday 22 February 2016

BODI YAMSIMAMISHA KAZI MHARIRI MTENDAJI.

BODI ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali(TSN), imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji Bw; Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.


Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo ni kutokea kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Warioba amesema nafasi ya mhariri mtendaji huyo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.


"Kumekuwa na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza ".Alisema Prof Warioba.

Katika hatua nyingine Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.

Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21 kuacha kazi.

"Nataka Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi." Alisema Mhe Nape.

Hata hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa.

No comments:

Post a Comment