Pages

Friday 19 December 2014

Mfahamu mzee mwenye wake 6,watoto 57 wajukuu 200 na vituku 70.

Mzee Nterege Nyigana Mutari ana umri wa miaka 103 ni mtu ambaye ni wapekee na alitahili kuwekwa katika kitabu cha maajabu duniani sababu amevunja rekodi kwa kuwa na watoto 57, wajukuu 200 na vituku 70.
hivyo kama hiyo haitoshi, unaamua kujenga shule
ili wapate elimu bora, tena katika shule hiyo
yenye wanafunzi 744, wanafunzi 200 wanatoka
katika familia yake, wakiwemo wajukuu na
vitukuu. Sasa mzee kama huyu, kwanini
asiwemo katika maajabu ya dunia?
Baada ya kufikiria mambo.
mengi.
Mzee Nterege ambaye ni mkazi wa
kitongoji cha Nyamaitagi, kijiji cha Nyamakobiti,
kata ya Majimoto Wilaya ya Serengeti mkoani ni wa kabila la
Wangoreme anaishi umbali wa kilometa 70
kutoka makao makuu ya wilaya ya Serengeti,
mjini Mgumu.

Historia ya Mzee huyo imejaa mengi yakiwemo
machungu na raha, lakini kwa upande wake
anasema vikwazo katika maisha ni jambo la
kawaida.
"Nina miaka 103, wajukuu zaidi ya 200 na
vitukuu zaidi ya 70, nilizaa watoto 57 lakini
ninachoweza kuieleza jamii ni kwamba watoto
wangu nimeamua kuwapa elimu bora kwa kuwa
elimu ndiyo ufunguo wa kila kitu hapa duniani,"
anasema Nterege.
Maisha yake
Nterege alizaliwa mwaka 1908 lakini akajulikana
kwa jina la "Reterenge'', jina ambalo anasema
alipewa na daktari raia wa Ujerumani.
Anasema alizaliwa katika eneo la Kyehonda -
Kimeli ambalo kwa sasa ni eneo la kijiji cha
Nyamutita na kwamba wakati huo baba yake
alikuwa na wake wawili.
"Kwa upande wa mama yangu tulizaliwa wawili
tu, mimi na dada yangu ambaye anaitwa
Nyakimaiga, mama yetu alikuwa mke wa pili wa
baba," anasema Nterege.
Anasema mwaka 1918 baada ya baba yake
kufariki dunia, ndugu wa baba yake walichukua
mifugo yote iliyoachwa na baba yake wakiwemo
Ng'ombe zaidi ya 100, na kuwanyang'anya
nyumba waliyokuwa wakiishi na mama yao.
"Walitufukuza pamoja na mama kwa kuwa
alikuwa mke mdogo wa marehemu baba,
walisema kuwa mama yetu wa kambo ambaye
alikuwa mke mkubwa ndio alikuwa na haki ya
kupata kila kitu. Kuanzia hapo tulianza kuishi
kwa shida."
Anasema baada ya tukio hilo alianza maisha ya
kujitegemea ambayo yalimfanya ashindwe
kwenda shule na kujikita katika kilimo na wakati
mwingine kufanya kazi ya kuchunga mifugo ya
watu mbalimbali ili kupata fedha za kuweza
kujikimu.
"Mwaka 1937 nilioa mke wa kwanza, Wansama
Moremi ambaye kwa sasa ni marehemu nilihamia
eneo la Nyamakobiti kuanza maisha mapya ya
ndoa…, mke wangu nilimtolea maali ya Ng'ombe
kumi niliowanunua baada ya kuuza Ulezi
niliolima kati ya mwaka 1935 na 1936," anasema
Nterege.
Wazo la kuwa na familia kubwa
Anasema katika maisha yake mapya baadhi ya
mambo yaliyokuwa yanamsumbua, ilikuwa ni
jinsi gani angeweza kupata watoto wengi kwa
kuwa alizaliwa yeye na dada yake tu.
"Wakati ule kuwa na familia au ukoo mkubwa
kilikuwa kitu cha heshima katika mila zetu,"
anasema Nterege.
Pia, anasema ukubwa wa familia ulikuwa
muhimu ili kuweza kupambana na vitendo vya
wizi wa mifugo ambapo mara kwa mara
kuliibuka mapigano ya kikabila kati ya kabila
lake na Wakulya na Wangoreme.
"Maisha ni mapambano. Nilianza kufanya
biashara ya mifugo mwaka 1940 nikishirikiana
na Chifu Makongoro wa Waikizu. Nilipata
Ng'ombe 800 wa kwangu mwenyewe ila kwa
sasa wamebaki 220 baada ya kuwapa watoto
wangu kwa ajili ya kuanza maiasha yao ya
kujitegemea,"
Kuoa
Akizungumza wanawake aliowaoa Nterege
anasema,
"Nilioa wanawake saba lakini niliodumu nao ni
sita, wanawake hao sita walizaa watoto 57, ila
watoto waliopo hai ni 37,".
Anaongeza, "Watoto wangu 20 walifariki
kutokana na kwamba wakati huo vituo vya kutoa
huduma ya afya vilikuwa mbali,".
Anasema kuwa ana wajukuu zaidi ya 200,
vitukuu zaidi ya 70 na anafafanua ," Wengine
siwatambui hata kwa majina,".
Anasema mwaka 1937 alimuoa mke wake wa
kwanza, Wansama Moremi, Gasawa Mayengo
(1939),Mandala mwita (1953), Nyamhanga
Nyamani (1963), Odela Osole (1969), Nyambura
Paka (1965) na Mkami Myangosira (1974)
ambaye waliachana bila kuzaa mtoto.
Anasema mpaka sasa wake zake walio hai ni
wawili ambao anaishi nao na anawataja kuwa ni
Nyamhanga Nyamani na Nyambura Paka.
Nterege anasema jambo kubwa analojivunia ni
kumwona mtoto wake wa mwisho, Julius
akisoma elimu ya sekondari ambapo alimaliza
mwaka juzi.
Anasema kaka yake Julius anayeitwa Nyamanko
alimaliza sekondari mwaka 1990, na wajukuu
zake watano nao wamemaliza elimu ya
sekondari ambao ni Gesile(2003), Bonifasi
(2009), Nyakimaiga (2011).
"Kuna mmoja anaitwa Nyamitari bado yupo
kidato cha tatu kwenye shule ya Sekondari ya
Busawe, shule ambayo nilichangia ujenzi wake,"
anaeleza kwa kujivunia kwa kitendo chake cha
kuchangia maendeleo ya jamiii.
Anasema watoto wake 19 ambao wako hai ni wa
kike na wa kiume 18. Mtoto wake wa kwanza
anaitwa Mayengo na alizaliwa mwaka 1942.
Kujenga shule
Mzee Nterege ambaye bado ana kumbukumbu ya
mambo mengi licha ya kuwa na umri mkubwa
anasema kuwa mwaka 1988 baada ya kuona
wajukuu zake wakipata usumbufu wa kwenda
shule zilizokuwa vijiji vya mbali, aliamua kubuni
wazo la kuanzisha shule ya msingi kuondoa
usumbufu huo.
Anasema alianza ujenzi wa shule kwa kutumia
magari yake kubeba mchanga na kokoto huku
akiwahamasisha wakazi wa kijiji hicho kuchangia
ujenzi.
"Ilikuwa ngumu kuwashawishi kwa kuwa kipindi
hicho watu walikuwa hawapendi kuelezwa habari
za kuchangia fedha kwa ajili ya jambo fulani.
Anasema kwamba mwaka 1990 alifanikiwa
kumaliza ujenzi wa jengo la utawala kwa nguvu
zake pamoja na wananchi.
"Licha ya kuwa mimi sikusoma niliamua kujenga
shule ili wajukuu zangu wapate elimu. Elimu
ndiyo kila kitu. Huwezi kufanikiwa katika maisha
ya sasa bila elimu. Niliona wajukuu zangu
wasiposoma watakuwa watumwa na tegemezi,"
anaeleza Nterege.
Anasema mwaka 1991 shule hiyo ya msingi
iliyopewa jina la Nayamakobiti ilifunguliwa kwa
usajili namba PS 0904080 ikiwa na eneo la
ukubwa wa Hekta 9.5.
"Shule hii niliamua kuiita jina la kijiji badala ya
jina langu kwa kuwa sikutaka sifa katika suala
hili, mtu unatakiwa usifiwe ukiwa umekufa si
ukiwa hai," anasema Nterege.
Mkuu wa shule hiyo anasemaje
Akizungumzia historia ya shule hiyo mkuu wa
shule hiyo, Machumbe Mairo anasema kuwa
huwezi kuzungumzia maendeleo ya shule hiyo
bila kumtaja mzee Nterege.
Anasema shule hiyo ina wanafunzi 744 na
anafafanua kwamba pamoja na changamoto
zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na
uhaba wa walimu.
Pamoja na matatizo hayo alisema inafanya vizuri
ambapo wanafunzi wengi hufaulu kuendelea
kidato cha kwanza.
"Katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010 shule
hii imeweza kufaulisha wanafunzi 122 kwenda
sekondari, wasichana wakiwa ni 41 na 81
wakiwa ni wavulana," anasema Mairo.
Anasema wanafunzi 200 wa shule hiyo kati ya
wanafunzi 744 wanatokea katika familia ya mzee
Nterenge wa kiwemo wajukuu na vitukuu.
"Familia yake ni kubwa kweli yaani hapa kijijini
wako wengi. Ukienda vijiji jirani pia wapo,"
anasema .
Chanzo:MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment