Pages

Friday 9 October 2015

Magufuli atua Bagamoyo na ahadi kemikemi za maendeleo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli aendelea na kampeni nakusema iwapo watanzania watampa ridhaa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataifanya Bagamoyo kuwa na maendeleo nakuahidi kuweka bandari eneo hilo la Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo ameyasema leo katika wilayani Bagamoyo katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo amesema bandari na viwanda hivyo vitasaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana.


"Tutafanya ujenzi wa viwanda vya kisasa katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano na tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi yote," amesema Dk. Magufuli


Aidha John Pombe Magufuli aliwanadi wagombea ubunge wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa na jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni huo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment