Pages

Tuesday 13 October 2015

TANZIA:WAZIRI ABDALAH KIGODA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki dunia nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge zinasema kuwa, Waziri Kigoda amefariki jana majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Appolo nchini India.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa kuhusu taratibu za msiba huo, ikiwa ni pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu na mipango yote ya mazishi zitaendelea kutolewa na Serikali pamoja na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu kadri zitakavyoendelea kupatikana.

Waziri huyo alipelekwa India kwa matibabu mapema mwezi Septemba
#Mwananchi

No comments:

Post a Comment